Shilole Kufunga Ndoa na Ashraf Uchebe Desemba 20
Hatimaye nyota wa filamu na muziki nchini, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole ametangaza kuwa atafunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.
Shilole amesema atafunga ndoa na mpenzi wake wa sasa Ashraf Uchebe Desema 20 siku ambayo ataadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kuibuka utata kufuatia akaunti moja ya Instagram inayosomeka jina la Uchebe kuandika maneno ya kumkejeli mwanamuziki huyo.
Shilole ameeleza kuwa akaunti hiyo si ya mpenzi wake bali imetengenezwa na watu wasiowatakia mema.
"Mpenzi wangu hana akaunti, watu wanataka kutuharibia sasa nawaambia wameshindwa na tunafunga ndoa," amesema Shilole.
Post a Comment