Peter Msigwa azungumzia maendeleo ya afya ya Tundu Lissu

Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Katika
ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mbunge Msigwa amewataka watu
waendelee kumuombea Lissu aliyesafirishwa jana usiku kupelekwa kwa
matibabu katika Hospitali ya Aga Khan akitokea Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Dodoma.
Katika
hatua nyingine, Rais wa Chama cha Mawakili cha Kenya (LSK), Isaac Okero
amesema wanachama wa Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki leo
mchana wataenda kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika (TLS).
Post a Comment