Nisha: Sikutani na Mpenzi Wangu Nyumbani Kwangu
Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’. |
STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa, hana kawaida ya kuruhusu mpenzi wake kufika nyumbani kwake kwa vile anahofi a kumfundisha maadili mabaya mtoto wake ambaye hivi sasa ameshakua mkubwa.
Akizumza na Za Motomoto News, Nisha alisema kuwa, kubadilika kwa dunia ya sasa, kumesababisha watu kutoaminika hivyo tahadhari ya hali ya juu inapaswa kuchukuliwa kuhusu wapenzi wake kufi ka kwake hasa mwanaye Iptysam anapokuwepo.
“Kama ni boyfriend huwa tunakutana sehemu nyingine, lakini siyo nyumbani kwangu mwanangu akiwepo, maana sitaki akue katika maadili mabaya,” alisema Nisha
Post a Comment