ad

ad

Mkude Afunguka Sababu Ya Kukaa Benchi Simba

BAADA ya Jumapili iliyopita, kiungo na nahodha wa zamani wa Simba, Jonas Mkude kupata nafasi ya kuitumikia timu  hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Bara, ameweka wazi sababu inayomfanya akose nafasi ya kucheza mechi nyingi msimu huu. Tangu kuanza kwa michuano ya ligi kuu msimu huu,  Mkude ambaye alikuwa tegemeo la Simba katika nafasi ya kiungo msimu uliopita ambapo aliweza kuitumikia timu hiyo katika mechi 28 za ligi kuu kati ya 30, ameonekana uwanjani mara moja katika mechi tatu ambazo kikosi hicho kimecheza. 


Akizungumza Mkude baada ya kupata nafasi hiyo ya kuitumikia Simba kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita dhidi ya Mwadui FC, alisema sababu kubwa inayomfanya akose nafasi ya kucheza ni kutokana na hali ya ushindani wa namba iliyopo kwa sasa ndani ya kikosi hicho. 

Lakini pia aina ya mfumo ambao Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amekuwa akiutumia msimu huu. 

“Kuna sababu mbili ambazo zinanifanya nishindwa kucheza Simba, mfumo na ushindani wa namba hizi ndiyo zinanifanya niwe nje ya kikosi mara kwa
mara. 


“Zaidi ya hapo, hakuna kitu kingine na kama kipo basi mimi sikijui,” alisema Mkude ambaye pia katika mechi saba za kirafiki za timu hiyo za kujiandaa na msimu huu wa ligi kuu alifanikiwa kucheza michezo mitatu tu.

No comments

Powered by Blogger.