IGP Sirro Afunguka Shambulio la Lissu, Kutekwa Watoto Arusha (Video)
IGP Sirro.
Sirro amezungumzia juu ya mauaji ya Kibiti na kusema hali sasa ni tulivu na asilimia 90 ya wahalifu wameshakamatwa.
Pia amezungumzia juu ya kauli ya jana ya Rais Magufuli kuhusu kuwakamata waliotajwa kwa kashfa ya madini kwenye ripoti ya Biashara ya Tanzanite na Almasi na kusema kuna watu wameshakamatwa mkoani Manyara tayari huku akieleza kuwa tukio la watoto kutekwa Arusha kwa sasa watuhumiwa wameshakamatwa na mmoja wao ameshauawa huku upelelezi ukiendelea.
Akizungumzia suala la Tundu Lissu kupigwa risasi amesema wametuma wapelelezi wao wazuri kwenda Dodoma na lazima watawakamata, akaongeza kuwa itawezekana kama wananchi watawapa taarifa.
Jibu: Silaha iliyotumika Tundu Lissu ni SMG au SR, matukio mengi ya uhalalifu silaha hizi hutumika, zinaingizwa nchini na kutoka nchi jirani zenye vurugu, inatumika maeneo mengi nchini.
Swali: Kwa nini kupigwa risasi Tundu Lissu kumetokea eneo ambalo viongozi wa serikali wanakaa, hii inaleta taswira gani?
Jibu: Matokeohaya hayatokei porini, hutokea sehemu ambayo sehemu watu wanakaa, mfano mhalifu akitaka kuiba gari ataenda sehemu ambayo magari yanahifadhiwa. Tanzania sio kisiwa, haya matukiowanayaona nchi nyingine wanaiga na kuja kuyafanya huku pia.
Upelelezi juu ya kushambuliwa Tundu Lissu hatuwezi kusema umefikia wapi kwa sababu ni mapema sana. Nimelizungumzia kwa kifupi sana ili lisitoe mwanya kwa wahusika kujua tunachofanya.
Swali: Watuhumiwa waliotajwa jana kwenye ripoti ya madini kwa nini hawajaitwa kwa majina waje mmoja mmoja kwa DCI kama inavyofanyika wanaitwa kiujumla?
Jibu: Upelelezi una namna nyingi, iwe kwa jina moja moja au kwa ujumla haijalishi kikubwa ni wote waliotajwa wanaripoti, hata ambao hawajatwa kwenye ripoti ikigundulika wanahusika wataitwa pia
Swali: Kumekuwa na msuguano wa mara kwa mara katiya polisi na Tundu Lissu, kuna wahalifu walivaa nguo zinazoendana na sare za polisi walitaka kulichafua jeshi hili mnalizungumziaje?
Jibu: Kinachofanya uhalifu sio uniform, kinachofanya uhalifu ni mtu, mara nyingi tumekamata watu wanaovaa nguo zinazofanana na polisi, cha msingi ni tumkamate yule aliyefanya tukio.
Tunamkamata kamata Tundu Lissu kutokana na matendo yake, kutokana na sheria ilivyo na akikamatwa anapelekwa mahakamani, hapo kuna tatizo gani? Polisi tunatenda haki kwa raia yoyote na hatupo kwa ajili ya kumuonea mtu.
Swali: Kuna watu waliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kufurahishwa na Tundu Lissu kushambuliwa na kijana mmoja anajulikana kwa jina la Suleiman na DC wa Kilombero kuna ujumbe wao unasambazwa kwenye mitandao, je mmechunguza hili na mmekamata hao watu?
Jibu: Jeshi la polisi linafuatilia, mambo mengine hatutarajii kabisa, mwenzako amejeruhiwa halafu wewe uka comment kuonyesha furaha, hata polisi walipouawa 8 kuna watu walikuwa wanafurahia, wapelelezi wetu wanafuatilia kuonyesha kilicho nyuma ya furaha yao.
Swali: Tundu Lissu madai yake aliyosema kuna watu wanamfuatilia na kumtisha mliyafuatilia?
Jibu: Tundu Lissu akija mmuulize swali kuwa aliripoti kwa polisi? Mtu ukitishiwa unatakiwa kuripoti kituo cha polisi sio kwa wanahabari. Tundu Lissu ni mwanasheria anajua haki zake.
Post a Comment