Dk Mwaka Aibuka na Gigy Money...Gigy Afunguka Kuwa Walikuwa na Mahusiano Muda tu
![]() |
Dk. Juma Mwaka akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’. |
UMAARUFU WA DK. MWAKA
Dk. Mwaka alipata umaarufu mkubwa kupitia kituo chake hicho cha tiba ya asili kilichokuwa maeneo ya Ilala-Bungoni jijini Dar, sanjari na kudhamini shughuli mbalimbali za kijamii kabla ya serikali kufungia kituo chake hicho, Julai mwaka jana. Kabla ya kufungiwa, umaarufu wa Dk. Mwaka ulichochewa zaidi na udhamini aliokuwa akiutoa katika shindano la mpira wa miguu la Ndondo Cup na ukwasi wa nyumba na magari ya kifahari aliyokuwa anamiliki.
HABARI KAMILI
Mapema wiki hii, wanahabari wa Global TV Online wakiwa katika majukumu yao, maeneo ya Mwenge, walikutana na Gigy Money katika Saluni ya Dage kwa ajili ya kufanya naye kipindi kipya kinachotarajia kuanza kurushwa kesho (Ijumaa).
DK. MWAKA AIBUKA Wakati huohuo, mwanahabari mwingine wa Global TV alimwita Dk. Mwaka ashiriki katika kipindi hicho kutokana na uzoefu wa muda mrefu wa masuala ya saluni alionao. Dk Mwaka alikubali, akatia timu.

KIPINDI CHAANZA Kipindi hicho kinachohusu masuala ya urembo, kilianza kwa
wanahabari pamoja na Gigy kujipodoa katika saluni hiyo huku maswali ya hapa na pale yakiendelea.
GIGY AMVAA DK. MWAKA
Baada ya kipindi hicho kukamilika, Gigy alimvaa Dk. Mwaka na kuanza kumkumbushia urafiki wao waliokuwa nao kabla hata hajawa maarufu. “Jamani mimi na Dk. Mwaka tulikuwa na uhusiano mkubwa tu kipindi cha nyuma kabla hata sijawa maarufu. “Yani alikuwa ni zaidi ya rafiki. Alikuwa kama ndugu yangu wa damu sema sasa tulikuja kupoteana na kila mtu alikuwa akipambana na hali yake. “Unajua watu wengi wamenijuia mimi kipindi hiki tu, hawajui nilipotoka, nimekutana na mengi na nimekutana wengi,” alisema Gigy bila kufafanua.
MAPICHA PICHA Baada ya kukumbushiana uhusiano wao wa miaka ya nyuma, tukio lililofuata ni wawili hao kupiga picha za kumbukumbu huku Dk. Mwaka akionekana kutoa ushirikiano kama anayesema ‘nimekumisi kwa kweli jamani.’
MBWEMBWE ZA GIGY SASA
Kuonesha kwamba amemmisi, Gigy ambaye anafahamika kwa kuwa mcharuko alianza kumshika Dk katika sehemu mbalimbali huku akiomba apigwe picha za kumbukumbu alizoziita za ‘kimahaba niue’. Mdada huyu bila kuweka akilini kuwa aliyekuwa naye pale ni mume wa wake wawili, alianza kwa kumuegemea mgongoni, baadaye akamshika Dk Mwaka kichwani kabla hajamalizia na
pozi la kumwekea mikono yake kifuani.
DK. FULL KUTABASAMU
Wakati Gigy akiendelea na makeke hayo, Dk. Mwaka alionekana akiachia tabasamu mwanana kila mrembo huyo alipokuwa akibadilisha pozi.
WAIBUA MINONG’ONO
Wakati Gigy akiendelea kufanya makeke yake na Dk. kutoa ushirikano wa asilimia mia, iliibuka minong’ono kutoka kwa wapenda ubuyu waliokuwa saluni hapo. “Mh! Si bure hata kama wamekumbushiana urafiki wao lakini si kwa staili hii, hawa inaonekana kulikuwa na kitu huko nyuma. Si ajabu walikuwa wapenzi,” alisikika ‘snichi’ mmoja na mwingine akadakia: “Si unamjua Gigy lakini mambo yake?”
WENYEWE WAFUNGUKA
Kutokana na kuonesha kama ‘wanajuana sana’ hadi kuibua minong’ono, wanahabari wa Global TV walilazimika kuwauliza kama walipokuwa kwenye urafiki huo miaka iliyopita walianguka dhambini, kila mmoja alikanusha: “Hapana bwana ni urafiki wa kawaida tu, sema tulikuwa deep sana,” alisema Gigy.
MSIKIE DK. MWAKA
“Ni mshikaji tu wa kawaida hakuna chochote kilichovuka zaidi ya
hapo.
” DK. MWAKA ALIKUWA WAPI? Kabla ya kuibuka mapema wiki hii, Dk. Mwaka alikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko baada ya serikali kumfungia kliniki yake kwa kukiuka masharti na kutoa huduma kinyume na usajili wake.
CREDIT: GAZETI LA AMANI
Post a Comment