DAKTARI WA HOSPITALI YA AGA KHAN ASHANGAA MANJI KUUGUA MOYO KATIKA UMRI MDOGO
Mshtakiwa
Yusuph Manji anayekabiliwa na shtaka la matumizi ya dawa za kulevya,
akijadili jambo na Wakili wake Hajra Mungula kabla ya kupanda kizimbani
kwa ajili ya kuanza kujitetea.
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Daktari
bingwa Wa magonjwa ya moyo wa Hospital ya Aga Khan, Prof. Mustapha
Bapunia (62), ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa,
inashangaza, Manji katika umri mdogo alionao anamatatizo sugu ya moyo
ambayo yanampasa kujilinda sana.
Dkt,
huyo ambaye ni shahidi Wa tatu upande wa utetezi katika kesi ya matumizi
ya dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufu
Manji amedai hayo leo wakati à kitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Cyprian Mkeha.AkiongozwÃ
na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, shahidi Hugo amedai, Manji ana
vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba ni lazima ajiangalie sana
kwasababu anaweza kufa muda wowote.
Amedai katika umri mdogo alionao Manji kuwa na vyuma vinne kwenye moyo inashangaza sana na kitaalamy anapaswa kujiangalia sana.Amedai
Februari mwaka huu Manji alipelekwa hospitalini hapo akiwa anasumbuliwa
na maumivu kwenye moyo ambapo kutokana na historia ya ugonjwa
iliyotolewa na manji mwenyewe na kwamba aliwahi kuzibuliwa mishipa ya
moyo mitatu ilizibuliwa India, Dubai na Marekani lakini pia bado alikuwa
akipata maumivu inaonyesha kuwa anatatizo sugu la moyo.
Alidai
kuwa hata baada ya kumfanyiwa uchunguzi ilionekana kuna mshipa mwingine
ulioziba licha ya ile iliyozibuliwa kuwa wazi lakini walipotaka
kumzibua alikataa na kuomba apewe dawa kwasababu familia yake na
matibabu yake yapo marekani.
Baada
ya vipimo walimshauriwa kutumia dawa za aina nne ambazo ni muhimu sana
kwasababu ya umri wake mdogo ili ya kupunguza maumivu makali. Kwani
vipimo vinaonyesha Manji ana maumivu sugu ya mgongo na kukosa usingizi
ambapo alipewa dawa za kupunguza maumivu (Benzodiazepines)ambazo
zinatotewa kwa cheti cha daktari lakini baadae tatizo lilijirudia na
kurudishwa tena february 24,2017 saa mbili usiku ambapo majibu ya vipimo
vilionyesha kapata mshtuko, wakarekebisha na kumuwekea chuma na
kuruhusiwa Machi 14,2017.
"Sisi
kwa wagonjwa wa moyo tunatumia Morphine ambayo inasaidia kupunguza
maumivu makali na dawa kutoka nje zinaruhusiwa lakini ukiwa na mzigo
mkubwa lazima uwe na kibali cha TFDA".Katika
utetezi wake Manji alikataa mashtaka ya kutumia dawa za kulevya na
kudai kuwa amechafuliwa sana, kwani dawa ambazo zinatajwa kwenye hati ya
mashtaka, Morphine na Benzodiazepines ni sehemu ya dawa zake anazotumia
na hata siku aliyohojiwa Polisi alikuwa akitumia dawa hizo ana
uthibitisho wake.
Aidha
aliomba kutoa uthibitisho huo mahakamani kama kielelelezo na kuongeza
kuwa Uthibitisho wa dawa hizo ulifika kwa njia ya e-mail na sekretari
wake ndio alitoa nakala wakati akiwa Hospital ya muhimbili .
Alidai
baada ya sekretari wake Maria kupriti ndio akampatia ndipo wakil wake
Hajra kuomba karatasi hiyo ipokelewe kama utambulisho mahakamani hapo.Manji
alizitaja aina ya dawa anazotumia kuwa ni Aderall, Vicoean,
Bercoced,Xanax na Zyban, ambapo alidai Aderal kwaajili ya kuzuia fikra
zisipotee akiwa anafanya kazi.
"Dawa
hiyo kwa tanzania inajulikana kama nacotin ambazo anakunjwa kila siku na
dawa hizo nazipata za siku 90 nikiwa tanzania na nikiwa marekani napewa
za siku 30" alidai.
Amedai
polisi walienda kukagua nyumbani kwake pia ambapo walichukua Kompyuta,
Viza Card, Credit Card, Bima na saa ambavyo hawajamrudishia hadi leo na
kudai alishangaa anakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya lakini Polisi
walichukua vitu vingine ambavyo havihusiki.
" Hii
kesi inatokana na ugomvi wa kibiashara na niq mchezo mchafu, kwani
hakuna asiyejua kama walikuwa anagombania Kampuni ya Tigo"alidai na
kuongeza."Kesi
hii menisababishia athari kubwa sana, binafsi Nimejiuzulu klabu ya
Yanga kwa sababu ya dawa za kulevya na niliandika barua kwa Mkuu wa
wilaya ya Temeke kuachia udiwani"alidai.
"Heshima
yangu imeshuka hata mbele ya viongozi wakubwa akiwemo Rais mstaafu
Benjamin Mkapa na Raila Odinga ambao wananifahamu, hivyo naona aibu".Aidha
Manji alipoulizwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis kwamba
anajua dawa za kulevya zinakaa muda gani mwilini alijibu ndio.
Alimuuliza
Manji aliomba vibali vya kutumia dawa zake ambazo nchini hazipo na
kujibu "Ingekuwa biashara ningeomba, lakini hizi natumia kama dawa hivyo
zinakibali na uthibitisho maalum kutoka hospitali niliyopewa".
Pia alidai alishapewa onyo aache kutumia sigara lakini amejiaribu bila mafanikio.Pia
shahidi wa nne katika kesi hiyo, Dr Khan aliieleza mahakama kuwa yeye
ni daktari wa watoto na familia na amekuwa akimtibu Manji toka akiwa na
miaka mitatu na hajawahi kuona kiashiria cha kutumia dawa za kulevya.
Post a Comment