ad

ad

Chuchu Hans: Sitamani Kuolewa Na Ray Ng’o!


CHUCHU Hans ni mmoja wa mastaa wa filamu ambao wanafanya vizuri kupitia tasnia hiyo na kama ukibahatika kuangalia moja ya kazi zake, utakiri niyasemayo. Pia si msanii tu wa filamu bali yupo vizuri kwenye kuigiza hata kucheza muziki mbalimbali na ndiyo maana akiwa katika mashindano ya urembo wa Miss Tanzania miaka hiyo, aliibuka mrembo mwenye kipaji cha kucheza muziki (dancing talent). 

Staa huyu ambaye miezi nane aliyopita alibahatika kupata mtoto wa kiume aliyempa jina la Brian aliyezaa na mwigizaji nguli wa kiume Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameweka wazi maisha yake ya sasa hivi pamoja na kazi zake;
Over Ze Weekend: Vipi maisha ya ulezi maana umepumzika kwa muda mrefu?
Chuchu: Naendelea vizuri na ninayafurahia maisha haya kwa sababu kuna vitu vingi ninajifunza hasa kuwa jasiri kama mama.
Over Ze Weekend: Mnaendeleaje na maisha ya kimapenzi wewe na mzazi mwenzio Ray?
Chuchu: Tupo vizuri, Ray anasimama kama baba na mimi ninasimama kama mama kwa mtoto wetu.
Over Ze Weekend: Kulikuwa na tetesi za kufunga ndoa kabla hata ya kujifungua, vipi ishu hiyo bado ipo?
Chuchu: Hakuna ishu kama hiyo tena.
Over Ze Weekend: Ni kwa nini au nini kimetokea?
Chuchu: Hakuna lililotokea ila tu sitamani kuolewa naye (Ray) tena, nafikiri ni kwa sababu tumejuana sana na kila mtu amemzoea mwenzake.
Over Ze Weekend: Mbona kuna tetesi kuwa mnaishi pamoja?
Chuchu: Hapana, wala haijawahi kutokea, yeye anaishi kwao na mimi ninaishi kwangu.
Over Ze Weekend: Ulijisikiaje kwa mara ya kwanza, Ray alipokuanika kama mpenzi wake na huko nyuma hakuwahi kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi?
Chuchu: Najisikia furaha na ndiyo maana niliamua kumpa zawadi ya mtoto kwa kuwa umri wake niliona unaenda na watu walishaanza kumsema tofauti maana kumzalia mtoto mimi ni kumpa zawadi yeye.
Over Ze Weekend: Huna mpango wa kuongeza naye mtoto mwingine?
Chuchu: Hapana, zamani nilifikiria hivyo, lakini hilo wazo hakuna tena.
Over Ze Weekend: Kwa nini umeamua kuahirisha mpango huo?
Chuchu: Sina hata sababu maalum, nimebadili tu mawazo.
Over Ze Weekend: Kutokana na kazi zenu na baba watoto wako ni moja na unajua mambo mastaa, vipi hujisikii wivu na yeye?
Chuchu: Hapana, sina wivu kabisa, roho yangu ni ya Kizungu.
Over Ze Weekenda: Mara nyingi mastaa watoto wao wakifikisha arobaini ndiyo huwa wanawatoa nje, lakini kwa nini mpaka leo, miezi nane hujamuonesha mtoto wenu?
Chuchu: Huo ni uamuzi wa baba yake maana kila kitu nimemuachia baba yake.
Ijumaa Wikienda: Kuna kipindi mlianzisha kampuni yenu ya CHURA (Chuchu na Ray), vipi imeishia wapi?
Chuchu: Ipo, ninaiendesha mimi.
Over Ze Weekend: Baada ya kujifungua tayari umesharudi kazini?
Chuchu: Ndiyo, nimeanza kufanya kazi hata za watu, wakiniita ninafanya na pia sasa hivi napika vyakula, ninasambaza kwenye ofisi mbalimbali.
Over Ze Weekend: Najua Ray amekukuta na watoto wako wengine wawili, je, anawachukuliaje?
Chuchu: Anawachukulia kama watoto wake kabisa.
Over Ze Weekenda: Vipi kwa upande wa wakwe zako, umepokelewa vizuri?
Chuchu: Sana na wananipenda mno.
Over Ze Weekenda: Kulikuwa na tetesi kuwa ulikuwa na bifu na msanii Johari, vipi limeisha?
Chuchu: Sijawahi kuwa na mgogoro naye na tupo vizuri tu.
Over Ze Weekend: Nakushukuru sana Chuchu kwa ushirikiano wako.
Chu-chu: Asante na karibu tena.

No comments

Powered by Blogger.