Wapigadebe 150 Watiwa Mbaroni Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, limetangaza kukamata watu wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi
17 mwaka huu, kwa makosa ya kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali
ya jiji katika vituo vya mabasi.
Wakati akizungumza na wanahabari
jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa
kufuatia misako na operesheni kali iliyofanywa na polisi, na kwamba
watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
“Stendi ya mabasi ya Ubungo
walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12, Tandika 16, Mnazimmoja 6,
Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema.
Katika hatua nyingine, Kamanda
Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati tofauti ilikamata
watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kujihusisha na
biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia sialaha na utapeli,
kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya gongo.
“Katika operesheni hii kali ambayo
ni endelevu, jumla ya kete 96 za dawa ya kulevya, misokoto ya bangi
107, gongo lita 60 zilikamatwa. Tunaomba raia wema kuendelea kutoa
taarifa za wahalifu ili tuwakamate na hatua kali za kisheria zifuatwe
dhidi yao,” alisema.
Alisema watuhumiwa wote wanaendelea
kuhojiwa kulingana na makossa yao na kwamba upelelezi ukikamilika
watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.
Post a Comment