WALICHOPITISHA WANACHAMA 1,216 WA SIMBA KWENDA KWENYE MABADILIKO, HIKI HAPA
Wanachama 1,216 wa klabu ya Simba, leo wamepitisha uamuzi wa klabu yao kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa hisa.
Mwanachama mmoja pekee katika mkutano huo, ndiye alionyesha hisia zake kwa kupinga mfumo huo.
Wanachama
bado wataendelea kubaki kuwa wamiliki wa klabu hiyo kwa asilimia 50
huku wawekezaji nao wakilimiliki kwa asilimia 50 pia.
Mbadiliko
yaliyopitishwa na wanachama wa Simba yako hivi, wanachama watamiliki
klabu yao kwa 50% huku 50% zikilikiwa na wawekezaji.
Wawekezaji au mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Sh bilioni 20 katika uwekezaji huo sawa na wanachama.
Kwa
wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao
watatakiwa kuchangia Sh bilioni 4 tu ambazo nia silimia 10 huku 40
ambayo ni bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao.
Suala
la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati baada ya watu kujitokeza,
nayo itaandaa mkutano kuwaita wanachama kuwaeleza waliojitokeza katika
uwekezaji ni akina nani.
Wawekezaji wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.
Post a Comment