Hamisa Mobeto na Zari The Boss Lady Kimenuka! Kisa Kipo Hapa
HALI si shwari kati ya mwanamitindo matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki ambaye ni mzazi
mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah hassan ‘Zari The Boss Lady’, kisa
kikielezwa kuwa ni mtoto.
Wakati mtoto huyo wa Mobeto aliyepewa jina la baba
mzazi wa msanii huyo akitimiza siku 14 leo Jumatatu, uzao huo umesababisha
Mobeto kuibuka na kicheko kwa kuungwa mkono na Wabongo huku Zari akidaiwa
kuambulia kilio kutokana na kushambuliwa mitandaoni.
Mara tu baada ya Mobeto
kujifungua mtoto huyo Agosti 8, mwaka huu, Zari alitokwa na povu ambalo siyo la
nchi hii huku akipiga mkwara kuwa asihusishwe na mtoto huyo wa ‘bitch’
(malaya), kauli ambayo aliitoa kupitia ukurasa wake unaotambuliwa kwenye
Mtandao wa Instagram.
Kilichofuatia ni majibizano ya mashabiki wa Mobeto na
wale wa Zari ambapo kila upande ulikuwa ukivutia upande wake, lakini pande zote
zilichukizwa na neno ‘bitch’ ambalo ni tusi lililotumiwa na Zari kwenda kwa
Mobeto ikielezwa kuwa lilitokana na hasira.
JINA LA BABA MkWE Wakati mambo yakiwa hayajakaa
sawa huku mtoto huyo wa pili wa Mobeto akiibua tafrani ya
aina yake mitandaoni, mwanamitindo huyo aliibua lingine baada ya kumpa mtoto
huyo jina lililodaiwa kuwa ni la baba mkwe wa Zari. Inasemekana kwamba, jambo hilo
ndilo linalodaiwa kuthibitisha kuwa Mobeto amezaa na mwanaume huyo hivyo kuibua
shangwe kwa Wabongo na kumuongezea machozi Zari.
Ilielezwa kuwa, jina hilo,
ndilo lililomaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa
mtoto huyo.
Awali, Mobeto alifungua akaunti kwenye Mtandao wa Instagram kwa
jina ‘Tanzania Baby’, lakini baadaye wiki iliyopita alibadilisha jina hilo
ambapo hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, akaunti hiyo ilikuwa ikikaribia
kuwa na wafuasi (followers) laki moja.
MAMA MZAZi NA DADA MTU
Tukio lingine lililoibua gumzo juu ya
mtoto huyo ni kufuatia kitendo cha mama mzazi wa jamaa huyo na dada yake
kuonekana kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye hospitali ambayo Mobeto
alijifungulia, ikidaiwa kuwa walifuata damu yao ambayo ni nzito kuliko maji.
Hata hivyo, jambo lingine lililozungumzwa zaidi ni kitendo cha jamaa huyo
kumkana Mobeto ikidaiwa kuwa alilenga kumpooza Zari ambaye inasemekana jambo hilo lilimtibua mno
na kumtaka jamaa huyo aliyezaa naye watoto wawili kukanusha kuzaa na Mobeto.
MOBETO APIGWA STOP
Katika mazingira hayo, mtu wa ndani ya
familia ya mwanaume huyo alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa Mobeto
amepigwa ‘stop’ (marufuku) kufanya mahojiano na waandishi wa habari. Hata
hivyo, Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa Mobeto, maeneo ya Mbezi-Beach
jijini Dar ambapo mara baada ya kujitambulisha lilifungiwa mlango wa geti kwa
madai kwamba, waandishi hawahitajiki.
WAZAZI FULL RAHA
Kwa upande wao, wazazi wa mwanaume huyo
anayedaiwa kuzaa na Mobeto, wamepokea baraka hiyo kwa mikono miwili huku babu
mtu akifurahia zaidi mtoto huyo kupewa jina lake.
40 YA kiShiNDO Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili
muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kwamba, familia ya Mobeto yaani
mama yake ipo kwenye mipango kabambe ya kuandaa 40 ya mtoto huyo kwani itakuwa
haijawahi kutokea Bongo. Tusubiri
Chanzo: Wikienda
Post a Comment