Tundu Lissu Aitisha Mgomo wa Mawikili Nchi Nzima
Baraza
la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili
nchi nzima kutokwenda mahakamani Jumanne na Jumatano kama njia ya
kupinga Kampuni ya Immma Advocate kuvamiwa.
Akizungumza
jana Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema uamuzi huo umefikiwa
jana na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.
Alisema mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.
Alisema baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.
Lissu
alisema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama
kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho
vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.
Alisema
baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi
la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.
Lissu
aliwataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya
wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea
wananchi.
Lissu Ataka Mawakili Wasiende Mahakamani Jumanne Na Jumatano by on Scribd
Post a Comment