TFF yaomba radhi kwa makosa ya kiuandishi kwenye Ngao ya Jamii Waliyopewa Simba Jana
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeomba radhi wanafamilia wote wa
mpira wa miguu nchini kutokana na makosa ya kiuandishi yaliyoonekana
kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017
kwa klabu ya Simba.
Ngao
hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na
Yanga SC zote za Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa ngao hiyo.
Makosa yaliyoonekana katika ngao hiyo ya jamii ni kukosewa kuandikwa kwa neno “SHIELD” ambapo liliandikwa “SHEILD” na hivyo kupoteza maana yake ya msingi.
Katika
taarifa ya TFF iliyotolewa leo Agosti 24 wamesema kwamba “Watanzania
hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea
vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo
wadau hawajapokea vema suala hili.”
Kuonyesha
kukerwa na uzembe huo uliofanywa na baadhi ya viongozi wake, Kaimu
Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi
waliohusika.
Mbali
na hilo, kiongozi huyo amewasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha
ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu
sahihi.
Uongozi wa TFF umesisitiza kuwa hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
Post a Comment