Breaking News: Chadema Waitaka Polisi Kumwachia Lissu na Kumkamata Ngeleja
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya Baraza la Vijana
(Bavicha), kinatarajia kufanya maandamano ya amani nchi nzima, Agosti
31, 2017 (Alhamisi) kwa lengo la kuishinikiza serikali kutekeleza sheria
na haki za binadamu kwa haki sawa.
Pia wanatarajiwa kuwafundisha vijana kulaani na kuzuia uvunjifu wa sheria, popote unapotokea nchini kwa madai kwamba Jeshi la Polisi limeshindwa kufanya kazi yake kwa hiyo lazima wanachama hasa vijana wachukue jukumu hilo.
Pia Chadema kimesema kwamba kitendo cha polisi kumkamata Lissu, ni uonevu wa hali ya juu kwa sababu hajafanya kosa lolote, watu wenye kesi ni wale walioiba fedha za Escrow lakini bado wanaendelea kudunda mitaani. Chama hicho kimeenda mbali kwa kusema, kwa kuwa sheria inamruhusu hata mtu binafsi kumkamata mhalifu, wao watafanya kazi ya kuwakamata watuhumiwa wa Escrow, akiwemo William Ngeleja, Anna Tibaijuka, Andrew Chenge na wengine wote wanaotuhumiwa.

Post a Comment