ad

ad

Tambo za wachezaji, Makocha Yanga, Simba Ngao Ya Jamii



MI A M B A ya soka nchini, Simba na Yanga, inatarajia kukutana leo Jumaano katika Uwanja wa Taifa, Da es Salaam kuondoa ubi¬shi unaoendelea kwa sasa.
Mchezo huu ni wa Ngao ya Jamii ambao u n a a s h i r i a kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu, i n a y o t a r a jiwa kuanza k u t i m u a vumbi Agosti 26 kwa timu 16 k u s h u k a dimbani.
C h a m pioni Jum a t a n o l i n a k u letea tambo mbalimbali za wachezaji na m a k o c h a kue l e k e a m c h ezo huo u t a k a oanza kup i g w a saa 10:00 jioni leo.
SHIZA KICHUYA
“Tumejiandaa vizuri na mchezo huo kwa kuwa kikosi chetu kipo vizuri na tuna¬hitaji kushinda.
“Kwa upande wa wachezaji hatuna mchezaji atakayetusumbua katika mchezo huo zaidi ya Ibrahim Ajibu ambaye kiwango chake tunakifahamu vizuri hakuna asiyekijua.”
HARUNA NIYONZIMA
“Siku zote mechi ya Simba na Yanga ni kubwa na ni ngu¬mu, na si kwa sababu nipo huku ndiyo niseme hivyo, hata nilivy¬okuwa Yanga mechi hii tulikuwa tuki¬ichukulia kwa umakini wa hali ya juu.
“Tunahitaji kujipanga ili tuweze kushinda mchezo huu, nimejiandaa vizuri ili niweze kuisaidia timu yangu iweze kushinda.”
NADIR HAROUB ‘CANNAVARO’
“Derby ya Simba na Yanga itakuwa nzuri na siku zote mchezo huu hauwezi kuutabiri, yeyo¬te atakayefanya vizuri atashinda, tusubiri dakika 90.”
ABDALLAH SHAIBU ‘NINJA’
“Watu wanaoongea vibaya kuhusu mimi, basi wasubiri timu yao tutakapokutana Taifa, wasubiri kuona muziki wangu.”
GADIEL MICHAEL
“Sina wasiwasi wowote na Simba kuelekea katika mchezo huu, kutokana na maandalizi makubwa tuliyoyafanya.
“Tupo katika maandalizi makubwa sana, naamini Sim¬ba hawana pa kutokea, timu yetu ipo vizuri kupambana na timu yoyote kwa sasa na si Simba pekee.”
EMMANUEL OKWI
“Naamini wapinzani tukiku¬tana nao tutawafunga mape¬ma tu kutokana na kikosi chetu kukamilika kila idara, kwa maana kwamba kila mmoja wetu anatimiza maju¬kumu yake ipasavyo.”
GEORGE LWANDAMINA
“Huku sisi tupo vizuri, tu¬naendelea na mazoezi kama kawaida, kikubwa ambacho naweza kusema ni kwamba vi¬jana wangu kila siku wanazidi kuwa imara na kunipa matu¬maini ya kufanya vizuri dhidi ya Simba.
“Kwa namna siku zinavyozi¬di kwenda, naona tupo tayari kwa mchezo huo, wapinzani wetu waje tu tupambane.”
JOSEPH OMOG
“Kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya kucheza na Yanga kwa sababu kila ambacho nili¬panga kukitoa kwa wachezaji kimekamilika na wamekishika kwa jinsi ambavyo nataka.
“Nikwambie tu kuwa hatuna presha na wapinzani wetu kwa sababu natambua tume¬shacheza nao na tumepata matokeo mazuri mbele yao, imani yangu ni kwamba lazi¬ma tutapata matokeo mazuri mbele ya wenzetu hao.”

No comments

Powered by Blogger.