SIMBA YAWASAMEHE WANACHAMA WAKE 71
UONGOZI wa Simba jana Jumapili uliridhia kuwasamehe waliokuwa
wanachama wa timu hiyo 71 wa Tawi la Simba na Maendeleo maarufu kama Simba Ukawa
baada ya hapo awali kuwafuta uanachama kwa kosa la kufungua kesi mahakamani.
Suala la kuwafungulia wanachama hao liliafikiwa jana na
wanachama wa klabu hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar.
Ili kuwarejesha kundini rasmi, kamati ya utendaji ya klabu
hiyo imewataka wanachama hao kufuta kesi yao ambayo walifungia wakipinga uchaguzi
uliowaingiza madarakani viongozi wa sasa wa Simba chini ya rais wake, Evans Aveva.
Post a Comment