Kimenuka: Mama Diamond Achukua RAV 4 Ya Hamisa Mobetto (Video)
BADO mrembo aliyezaa na Mbongo Fleva, Hamisa Mobeto ameendelea kutengeneza vichwa vya habari, safari hii, gari lake aina ya Toyota Rav 4 alilopewa na msanii huyo, linadaiwa kuibua zengwe kwa kile kinachoelezwa kuwa ilikuwa msanii huyo ampe mama’ke, akabadilisha maamuzi ghafla na kumpa Mobeto.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na familia ya Mobeto kimenyetisha kuwa, msanii huyo aliagiza gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tano kabla ya Mobeto kujifungua na ilikuwa amzawadie mama yake mzazi
. “Yule msanii alikuwa anataka kumpa ile Rav 4 mama yake sasa ilipotua nchini ndiyo wakati ambao Mobeto alikuwa amejifungua kwa hiyo akaona bora ampe mzazi mwenziye huyo mpya kwanza halafu mama yake akaahidi kumuagizia gari lingine. “Sasa nasikia mama wa msanii hakufurahishwa na kitendo hicho.
Kidogo alimaindi kwani tayari yeye alishajiandaa ku-drive mkoko mpya. Akabaki anaumia na moyo wake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Hata pale mama wa msanii huyo alipoenda hospitali kumuona mjukuu wake kwa mara ya kwanza, alikuwa hana furaha sana lakini ndiyo hivyo, atafanyaje sasa wakati
aliambiwa amuwakilishe mwanaye ambaye alikuwa nje kikazi.”
MAMA MOBETO AFUNGUKA
Mama’ke Mobeto, Shufaa Lutigunga alipotakiwa kuzungumzia zengwe hilo, aliomba aachwe kwani kwa sasa mambo mengi sana yamezungumzwa kuhusu yeye na mwanaye ambayo yamesababisha usumbufu mkubwa. “Jamani wenzenu sasa hivi mambo yamekuwa mengi sana kuhusu mimi na mwanangu. Ngoja tupumzike kidogo jamani,” aliomba aachwe mama Mobeto.
Alipotafutwa Mobeto na mama wa msanii, simu zao ziliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni. Hivi karibuni, msanii aliyezaa na Mobeto, alifunguka mambo mengi redioni kuhusiana na uhusiano wake na mrembo huyo likiwemo suala la kumnunulia gari hiyo ya Rav 4.
Kama hiyo haitoshi, alisema aliteketeza fedha nyingi kulea tumbo kwa kumpa shilingi elfu 70 kila siku, baadaye akampa hela ya kujifungua shilingi milioni saba kisha alipojifungua, akampa shilingi laki tano.
Hata hivyo, baada ya kujifungua, msanii huyo alisema Mobeto alikuwa na tamaa ya kuomba apewe shilingi milioni laki tano kila wiki hali iliyomfanya msanii huyo azungumze na mwanasheria wake ambapo mwisho wa siku walikubaliana ampe shilingi laki mbili kila wiki.
Post a Comment