ad

ad

PICHA 3 SIMBA WAKIWA NA NGAO YA JAMII YAO... MO IBRAHIM KAIVUTA NGAO


 Wanamichezo wana style zao za kushangilia au kusherekea ushindi, katika kushangilia kwao kuna wengine hufikisha ujumbe fulani waliokusudia.

Kijana Ibrahim Mohamed ‘Mo’ alifunga penati ya ushindi kwa upande wa Simba na kupeleka shangwe Msimbazi kwa ushindi uliowapa Ngao ya Jamii wakati wakicheza na watani wao wa jadi Yanga.

Mo aliuweka mpira tumboni kama ishara ya mama mjamzito, shaffihdauda.co.tz haikuacha kumuuliza kwa nini ameamua kufanya hivyo au ndio anatarajia mtoto siku za karibuni?

“Ni kweli kwa sasa mimi ni ‘baba kija’ (baba mtarajiwa) Mwenyezi Mungu akijalia nitapata mtoto siku za karibuni ndio maana nimeamua kushangilia kwa style hii nikiwa ninaonesha upendo na kujali kwa mwenzi wangu ambaye ni mjamzito kwa sasa,” Ibrahim Mohamed.

Mo alitokea benchi na kuingia dakika ya 80 kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin, alipiga penati ya sita na kumfunga golikipa wa Yanga Youthe Rostand, penati ambayo moja kwa moja ikaifanya Simba kuwa bingwa wa Ngao ya Mii kwa ushindi wa penati 5-4.




No comments

Powered by Blogger.