SIMBA IMEINGIA KWENYE MFUMO MPYA, LAKINI MJADALA USIFUNGWE ILI KUBORESHA MAMBO
NA SALEH ALLY
WANACHAMA
1216 wa Klabu ya Simba, kwa pamoja wameamua kufanya mabadiliko ya
katiba katika suala la uendeshaji wa klabu yao. Kumbuka Simba imezaliwa
mwaka 1936.
Hakuna
ubishi, Simba pia ilihitaji mabadiliko kupitia katika maisha mapya ya
ushindani kwa kuwa hata baada ya kuzaliwa, ilipitia mabadiliko kadhaa
kufikia hapa ilipo leo hii.
Mabadiliko
yaliyofikiwa ni jambo la mpito wa maisha na wanachama waliofanya
mabadiliko wanapaswa kujipongeza lakini wakiamini kuwa kuna hatua nyingi
za kupitia kufikia kwenye mafanikio na ikiwezekana siku za usoni,
mabadiliko mengine.
Mfumo
wao unasema hivi; mabadiliko yaliyopitishwa na wanachama wa Simba yako
hivi, wanachama watamiliki klabu yao kwa 50% huku 50% zikibaki kuwa za
wawekezaji.
Wawekezaji watakuwa mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Sh bilioni 20 katika uwekezaji huo sawa na wanachama.
Kwa
wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao
watatakiwa kuchangia Sh bilioni 4 tu ambazo nia silimia 10 huku 40
ambayo ni bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao.
Suala
la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati baada ya watu kujitokeza,
nayo itaandaa mkutano kuwaita wanachama kuwaeleza waliojitokeza katika
uwekezaji ni akina nani.
Wawekezaji wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.
Kitu
kizuri zaidi ni kwamba wanachama wataendelea kuwa wamiliki wa klabu kwa
asilimia 50 na ninachotaka kuwakumbusha kwamba hakuna kitu ambacho
hakina matatizo.
Hii
ni safari mpya, wameingia katika mabadiliko na kikubwa wanachopaswa ni
kuendelea kujielimisha zaidi kuhusiana na mfumo huo ili kuweza kuutendea
haki kwa ajili ya kujipatia maendeleo.
Nasisitiza
waendelee kujifunza zaidi kwa kuwa wanapaswa kuhoji kuhusiana na mfumo
huo, wanapaswa kuwapa wawekezaji changamoto zenye mlengo wa kujenga ili
kufanikisha.
Wanachama
wa Simba hawapaswi kuamini kwamba kwa kuwa wamefanya mabadiliko, basi
wanapaswa kukaa kimya na kuacha mfumo ufanye kazi. Kuna mambo mengi ya
kujifunza na kuyafanyia kazi ili mabadiliko yawe na maana.
Wawekezaji
wanaokuja ni kina nani, kwa nini wanataka kuwekeza Simba, uwezo wao ni
upi, wanaweza kusaidia nini. Historia yao kibiashara ilikuwaje na
ikiwezekana ni vizuri kuhoji kuhusiana na nia yao ili kupata uhakika
zaidi.
Kuingia
katika mabadiliko ni kuingia katika changamoto mpya, kukabiliana nayo
ni lazima kujielimisha zaidi kwa lengo la kutaka kujua mambo zaidi ili
unapohoji unakuwa na uelewa zaidi wa jambo husika.
Ninaamini
wako ambao wameshiriki katika mabadiliko hayo lakini hawakuelewa zaidi
au hawakuelewa kwa asilimia 100. Huenda walifurahishwa na kusikia
mabadiliko yataisaidia Simba kuwa imara zaidi.
Wako
walioamini Simba ikiingia katika mfumo mpya, basi kazi yake itakuwa ni
kushinda kila mechi, kuifunga Yanga kila siku na hakuna atakayeifunga
tena Simba.
Ninaamini
wako wamefanya hivyo kwa kuwa wanaitafuta furaha ya ushindi na kufanya
vizuri wakitaka kuyakwepa maumivu ya kufungwa au kupoteza na kuzomewa na
watani wao Yanga na wengine.
Haya
yote yanaweza kuwa sawa lakini kwa kila mwanachama aliyehusika
kupitisha mabadiliko hayo jana, namuasa kukumbuka kujifuza zaidi au
kuhoji zaidi kuhusiana na mfumo huo ili awe sehemu ya mabadiliko kwa
sehemu ya kuyapitisha lakini kuyasaidia yafanye kazi akiwa anaelewa kwa
nini alifanya mabadiliko.
Kwa
upande wa viongozi, wasiwe na jazba, wawape nafasi wenye hamu ya kuhoji
wafanye hivyo. Wajibiwe kwa mlengo wa kujenga, si jazba au
kuwadhalilisha kwa kuwa wengi walitaka.
Mtu
mmoja amekataa katika mkutano wa jana ana haki, hivyo bado wako
watakaopenda kuhoji nao wasaidiwe kujua ingawa nao walenge mafanikio
badala ya vurugu. Kila la kheri.
Post a Comment