Magari ya viongozi wa Tume ya Uchaguzi yakiingia ukumbini hapo.
Maafisa wakuu wa serikali pamoja na mabalozi wameanza kuwasili ukumbi
wa Bomas ambako kuna kituo cha taifa cha kujumlishia na kutangazia
matokeo ya urais, ishara kwamba tangazo muhimu linasubiriwa.
Ukumbi ukiwa umeandaliwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed na washirika wengine wakuu wa Rais Uhuru Kenyatta wamewasili Bomas.
Viongozi wakiwasili.
Mabalozi wa Marekani na Uingereza pia wamewasili. Kunashuhudiwa
shughuli nyingi na usalama umeimarishwa pamoja na hali kuonekana
kubadilika katika ukumbi huo.
Hali ilivyo nje ya ukumbi huo.
Tume ya uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba inatarajia kupokea
matokeo yote kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.
Ukumbi
Mwenyekiti wa tume hiyo anatarajiwa kutangaza matokeo baadaye baada ya kuhakikiwa kwa fomu za matokeo. Matokeo ya awali kwenye tovuti ya tume hiyo yanaonesha Rais Kenyatta
akiongoza kwa takriban asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa dhidi ya Bw
Odinga.
Post a Comment