Majeruhi watatu ajali ya Wanafunzi Arusha Kurejea Nchini Kesho Kutwa
Watoto
watatu walionusurika kwenye ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya
Lucky Vincent ambayo ilipoteza maisha ya wanafunzi 32, wanatarajia
kurejea nchini August 18, 2017 baada ya kupatiwa matibabu Marekani.
Mbunge
wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa mstari wa mbele
kusimamia shughuli ya kuwasafirisha, amesema ratiba ya mapokezi itaanza
mapema zaidi ambapo itakuwa saa Moja asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro, ‘KIA’ ambapo Makamu wa Rais Samia Sulu Hassan
atawaongoza Watanzania.
”Watawasili
tarehe 18, 2017 wiki hii wakiwa wanaletwa na ndege ile ile
iliyowachukua na ratiba inaanza mapema kidogo saa moja asubuhi, wananchi
na wanafamilia wanatarajiwa wawe wamefika uwanja wa KIA, Kutakuwa na
viongozi mbalimbali na tunatarajia makamu wa Rais kuwa mgeni rasmi.”
Amesema Lazaro Nyalandu.
Post a Comment