ad

ad

JENNIFER WA KANUMBA ACHAFUKA MITANDAONI



Muigizaji Jennifer.
MTOTO ‘mtukutu’ aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu za marehemu Kanumba, Hanifa Daudi amekumbwa na kashfa ya kitapeli, kufuatia watu wasiojulikana kufungua akaunti feki ya jina lake kwenye Mtandao wa Facebook na Instagram na kuanza kuomba pesa kwa watu mbalimbali. 
Kanumba na Jenifer.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya watu wamekuwa wakimlalamikia  kwa tabia ya kuomba pesa kupitia mitandao ya kijamii, jambo ambalo liliwashangaza wengi. “Kuna watu wanatumia jina la Jennifer kwenye mitandao kutapeli hivyo wameondoa lawama kwa muigizaji huyo na badala yake wameanza kumkingia kifua, tofauti na zamani ambapo walidhani ni yeye kweli anayefanya utapeli huo, mwenyewe maskini amekuwa ni mtu wa kulia na kuumia kwa kashfa hiyo,” alisema mtoa habari wetu.JENNIFERMarehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Mwandishi wetu alizungumza na Jennifer na kusema: “Naumia sana jamani, hebu nisaidieni, mimi sina akaunti kwenye Facebook, ni juzi tu mama yangu alinishauri nifungue akaunti ya Instagram ili kujitofautisha na hao matapeli, lakini sina simu na hiyo akaunti siitumii niko huku Tanga masomoni, wanatumia jina langu kutapeli, eti wanajiita Hanifa Jennifer Kanumba na wanaposti picha zangu, kweli sijui wanazitoa wapi, naumia jamani aah.”

NA: BRIGHTON MASALU

No comments

Powered by Blogger.