MADRID YAITWANGA TENA BARCELONA, SAFARI HII 2-0, JUMLA 5-1, YABEBA SPANISH SUPER CUP
Real Madrid wameiangushia Barcelona
kipigo cha pili, safari hii ikiwa ni mabao 2-0 na kufanikiwa kubeba
ubingwa wa Spanish Super Cup.
Madrid iliitwanga Barcelona kwa mabao 3-1 nyumbani kwao Camp Nou, Barcelona.
Leo bila ya mshambuliaji wake, Cristiano
Ronaldo aliyelambwa kadi nyekundu katika mechi ya kwanza, Madrid
imeshinda kwa idadi hiyo ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu.
Marco Asensio alikuwa wa kwanza kuandika
bao katika dakika ya nne tu ya mchezo na Karim Benzema akapachika la
pili dakika ya 39 baada ya kumuibia mpira beki Samuel Umtiti wa
Barcelona.
Madrid imechukua ubingwa ikiwa na jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa mabao 3-1 ugenini Camp Nou.
Post a Comment