FUATILIA LIVE Yanayojiri Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kenya
IKIWA ni Agosti 8, 2017, takribani raia milioni 19 wa Kenya wanatarajia kupiga kura kuwachagua rais, magavana wa kaunti, wabunge, maseneta, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa kata.
Vituo karibu vyote vya kupigia kura vimefunguliwa rasmi tangu saa 12: 00 alfajiri, huku wapiga kura wakijitokeza vituoni kuanzia majira ya saa 9 usiku tayari kupanga foleni kwa ajili ya uchaguzi huo.
Kwa mara nyingine, Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee na Raila Odinga
wa Muungano wa Upinzani NASA, wanaonekana kuwa na ushindani mkubwa
katika kinyang’anyiro hicho. Kenyatta ni mtoto wa Rais wa kwanza wa
Kenya, Mzee Jomo Kenyatta naye Odinga mtoto wa makamu wa rais wa kwanza
Jaramogi Oginga Odinga.
Waziri awahakikishia Wakenya usalama wakipiga kura
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya
usalama nchini Kenya, hasa kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa
kati ya wagombea urais wawili wakuu huku wenzi wao wakiwa bado
wanakumbuka ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Aidha, hivi karibuni Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana. Wakati huo Kaimu Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa.
Aidha, hivi karibuni Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana. Wakati huo Kaimu Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa.
Post a Comment