ad

ad

FT: SIMBA 1-0 RAYON SPORTS, UWANJA WA TAIFA, DAR


Niyonzima.
FULL TIME
Dakika ya 90 + 3: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inapata ushindi wa bao 1-0.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.Simba na Rayon wakimenyana.

Dakika ya 88: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 86: Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Said Ndemla ambaye anapiga shuti kali linatoka nje.
Dakika ya 84: Simba wanamtoa John Bocco anaingia Laudit Mavugo.
Dakika ya 76: Manula yupo chini, inaonekana ameumia, anapatiwa matibabu. Mchezo umesimama kwa muda kisha ukaendelea.


Okwi akimtoka beki wa Rayon.

Dakika ya 75: Rayon wanaamka na kupata kona, inapigwa lakini Manula anadaka.
Dakika ya 75: Rayon wanaamka na kupata kona, inapigwa lakini Manula anadaka.
Dakika ya 69: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kichuya ambaye aliushindwa kurejea uwanjani, nafasi yake inachukuliwa na mkongwe Mwinyi Kazimoto.
Dakika ya 68: Niyonzima anapiga pasi nzuri kwa Okwi lakini anashindwa kuitumia vizuri.Bocco akisanuka.

Dakika ya 66: Shiza Kichuta ameumia mguu wakati anawania mpira na beki wa Rayon, anachechemea na kutoka nje.
Dakika ya 66: Mchezo una kasi kubwa, wachezaji wa Rayon wanaambiana kutulia kwa kuwa Simba wanashambulia kwa kasi.
Dakika ya 63: Simba wanapata kona, wanaanzisha kona fupi lakini walinzi wanaokoa.



Dakika ya 62: Simba wanaendelea kulishambulia lango la Rayon, wanapiga pasi nyingi, Niyonzima anashangiliwa kila napogusa mpira.

Dakika ya 59: Simba wanapiga pasi zaidi ya 1o, wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao, pasi ya mwisho inafika kwa Bocco anapiga shuti linatoka nje.
Dakika ya 55: John Bocco amefanya kazi nzuri, ameingia na mpira na kuwatoka walinzi wa Rayon lakini akashindwa kumalizia kazi nzuri aliyoifanya.


Simba wakipongezana baada ya kupata bao.

Dakika ya 52: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 48: Simba wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Simba wamefanya mabadiliko kadhaa, beki Mohamed Hussein ameingia pamoja na Haruna Niyonzima naye ameingia.Kikosi cha Rayon.

Dakika ya 45: Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.



Haji Manara akifurahia jambo na Waziri Mwigulu Nchemba (kulia).

MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, Simba inaongoza bao 1-0.
Dakika ya 45 + 3: Rayon wanapata faulo, nje kidogo ya lango la Simba, wanapiga lakini inaokolewa.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa aiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.Okwi akifurahia jambo na waziri Nchemba kabla ya mechi kuanza.

Dakika ya 43: Beki wa Simba, Mbonde anaumia wakati akiokoa mpira.
Dakika ya 40: Okwi anajaribu kupambana kutafuta nafasi ya kupenya kwa beki wa Rayon lakini anazuiliwa.


Kikosi cha Simba.

Dakika ya 36: Mchezo unaendelea kwa timu zote kuwa kwenye presha kubwa licha ya kuwa ni mchezo wa kirafiki.
Dakika ya 35: Kotei anachezewa vibaya inakuwa faulo kuelekea kwa Rayon.
Dakika ya 30: Rayon wanawapunguza kasi Simba lakini mambo yanakuwa magumu.
Dakika ya 25: Kichuya anacheza vizuri, anatoa pasi kwa Okwi lakini anachelewa, walinzi wanaokoa.

Dakika ya 20: Mchezo una kasi kwa timu zote, Simba hawataki kuupozesha mchezo.
Dakika ya 16: Mchezo unaendelea kwa kasi, mashabiki wa Simba wameongeza nguvu ya kushangilia.
Dakika ya 15: Mohamed Ibrahim anaipatia Simba bao la kwanza, alipata pasi kutoka kwa Okwi, akaachia shuti mbele ya walinzi wawili wa Rayon Sports.Mohamed Ibrahim.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dakika ya 11: Simba ndiyo ambao wanamiliki mpira muda mwingi na wanatumia mawinga wao kufanya mashambulizi.
Dakika ya 6: Washambuliaji wa Simba wanaonekana kuanza kwa kasi, wanafika langoni mwa Rayon mara kadhaa.
Dakika ya 4: John Bocco ameshaangushwa chini mara mbili.
Dakika ya 1: Simba wameanza kwa kupigiana pasi na timu zote zinaonekana kusomana.
Mchezo umeanza.
Timu zote zimeshaingia uwanjani, kwa jili ya kuanza mchezo huu.
Kwa sasa wachezaji wanapasha misuli uwanjani. Idadi ya mashabiki ni wengi. Kikosi kitakachocheza leo dhidi ya Rayon Sports kimeshatangazwa, ndiyo hicho kilicho kwenye picha:
Kikosi cha wachezaji wa Simba watakaotumika msimu wa 2017/18 kimeshatajwa, wametajwa mchezaji mmoja mmoja ambapo walikuwa wakiingia uwanjani baada ya kutajwa jina la Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.
Leo ndiyo ile siku ambayo Wanasimba wengi walikuwa wakiisubiria kwa hamu, timu yao kuelekea msimu wa 2017/18 inatambulishwa. Shughuli hii inafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA  | GPL

No comments

Powered by Blogger.