ESTER KIAMA AKWAA SKENDO YA MARINGO KWA WASANII
Ester Kiama.
Wakizungumza na Za Motomoto News huku wakiomba hifadhi ya majina yao, baadhi ya wasanii wa kike walisema msanii huyo anaringa na kujitenga kwani hata kwenye shughuli au matatizo ya wasanii wenzake haonekani kushirikiana nao jambo ambalo linawakera.
Baada ya kupata madai hayo, Ester alitafutwa na kupatikana ambapo alisema; “Nimesikia hayo madai kwamba ninaringa, sijui eti najisikia siku hizi, lakini siyo kweli kabisa, sema kuna vitu vinaniweka busy sana, hivyo nakosa hata muda wa kujichanganya na wasanii wenzangu.”

Post a Comment