Bulaya Aruhusiwa Kutoka Muhimbili

Mbunge
wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameruhusiwa kutoka katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja.
Bulaya
alikimbizwa Muhimbili kutoka tarime mkoani Mara baada ya kupata tatizo
la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini
Tarime. Alikuwa amelazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji
akipatiwa matibabu.
Mbunge
huyo wa Chadema, leo Agosti 28 ameruhusiwa kutoka hospitali na
amewashukuru madaktari wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kina.
Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.
“Kwanza
nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa
kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa
sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea na shughuli za
maendeleo,” amesema Bulaya.
Bulaya
aliwekwa rumande Agosti 18 baada ya kukamatwa na polisi akidaiwa
kuingia jimbo la Tarime kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa
mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za
msingi kwa mwaliko wa mbunge mwenzake Esther Matiko.
Post a Comment