Ebitoke : Ben Pol Ananipenda Kama Nilivyo
Msanii
wa vichekesho Anastazia Kisaveli alimaarufu kama Ebitoke ameweka wazi
jambo ambalo anavutiwa zaidi na Ben Pol na kusema ni vile msanii huyo
alivyompenda na kumkubali jinsi alivyo.
Ebitoke
ambaye inadaiwa anatoka kimapenzi na Ben Pol amesema hayo kupitia
kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio kinachoruka kila
Jumamosi na kudai Ben Pol hakumtenga wala kumdharau kutokana na kazi
yake hiyo bali alimkubali na kumuhakikishia kumpa support katika kazi
yake hiyo ili afanikiwe zaidi na zaidi.
"Kuna
watu wananitisha kweli wanakuja 'DM' wengine wananitukana, wengine hivi
wewe Ebitoke unaweza kuwa na Ben Pol? Hivi mimi wananionaje hawa watu
wasinichukulie poa poa.
"Tunachotarajia
sasa Ben Pol kwanza lazima anipe 'support' kwa kila kitu nachokifanya
na mimi lazima nihakikishe natimiza malengo yangu kwa sababu amesema
atanisapoti kuanzia kazi yangu nayofanya mpaka mbeleni kwa hiyo huyo ni
mwanaume wa kweli kwangu, ambaye amekubali kazi yangu nayofanya,
amenikubali jinsi nilivyo hajanibagua nimefurahi sana aliposema kuwa
lazima anipe nguvu kutumiza malengo yangu" alisema Ebitoke
Mbali
na hilo Ebitoke anasema kuna mambo mengi yeye na Ben Pol wameyapanga na
anaamini kuwa yatatimia mbele ya safari katika maisha yao ya kila siku,
ila anasema kaka zake yeye walimjia juu kuona hizo stori za mahusiano
na Ben Pol lakini baadaye walielewa kuwa anachofanya ni kutafuta maisha
hivyo ilibidi wamuache na kazi yake hiyo ya uigizaji na kuendelea kumpa
'Support'
Post a Comment