Alvaro Morata amejiunga na Chelsea atoa tambo Ya Kuisubiri Man Utd
Staa kutoka kwenye kikosi cha Real Madrid, Alvaro Morata, ambaye amejiunga na Chelsea.
TIMU nyingi za Ligi Kuu England zimeonekana kujiandaa vyema sana kwenye kipindi hiki cha usajili jambo ambalo linaonyesha kuwa msimu mpya wa ligi utakuwa moto wa kuotea mbali. Kila timu imeanza vyema maandalizi yake, ingawa usajili umeonekana kutikisa zaidi kwenye ligi hiyo kuliko nyingine nyingi.
Kati ya wachezaji mahiri ambao wanasubiriwa kuonyesha kazi yao ni staa kutoka kwenye kikosi cha Real Madrid, Alvaro Morata, ambaye amejiunga na Chelsea kwa kitita cha pauni milioni 70.6, zaidi ya shilingi bilioni 199. Wikiendi iliyopita staa huyo alianza kufanya mazoezi chini ya kocha Antonio Conte na kuonekana akiwa na furahaya hali ya juu, baada ya awali kutajwa sana kuwa angeweza kujiunga na Manchester United.
Kuondoka kwa mchezaji huyo kwenye kikosi cha Madrid kumemfanya kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane, alalamike kuwa ana uhaba wa washambuliaji kwenye timu yake na hivyo anatakiwa kufanya usajili wa kuziba mapengo. Morata ni kati ya wachezaji ambao wameshafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye soka pamoja na kwamba umri wake bado ni mdogo akiwa na miaka 24 tu, lakini ameshatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, La Liga pamoja na Ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia.
Alvaro Morata alipotua Chelsea.Kinda huyo baada tu ya kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo alisema wanachotakiwa kufanya ni kupambana kama timu ili waweze kutwaa makombe makubwa duniani likiwemo lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika mazoezi yake hayo ya kwanza, Conte alionekana kufurahia kila jambo ambalo lilikuwa likifanywa na mshambuliaji huyo, huku akimuita mara kwa mara na kumuelekeza jambo jipya la kufanya.
Mashabiki wa soka barani Ulaya na sehemu nyingine tayari wameonyesha kuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana kumuona staa huyo uwanjani na kipimo chake cha kwanza ulikuwa mchezo wa kirafiki jana kati ya timu yake dhidi ya Bayern Munich. “Siwezi kusubiri kuvaa jezi ya Chelsea, naipenda Ligi Kuu ya England kwa kuwa ni ligi kubwa duniani na nafahamu kuwa Chelsea ni timu kubwa duniani kwa sasa.
“Nasubiri kuona nini kitatokea, lakini ukweli ni kwamba natamani kuona nacheza mchezo wangu wa kwanza wa ligi, najua kuna siku nitacheza dhidi ya timu kubwa kama Manchester United, Manchester City, Liverpool na hata Arsenal, hii itakuwa siku muhimu sana kwangu,” alisema Morata anayevaa jezi namba tisa . Hata hivyo, ni lazima mchezaji huyo raia wa Hispania aonyeshe kiwango cha hali ya juu kama anataka kupata nafasi kwenye timu hiyo ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita.
Tayari wachezaji kadhaa ambao walikuwa hawana nafasi msimu uliopita wameanza kuonyesha makali yao akiwemo mshambuliaji Michy Batshuayi, ambaye alionyesha kiwango cha juu sana kwenye mchezo dhidi ya Arsenal wiki iliyopita na kufunga mabao mawili. Morata ambaye amefunga mabao tisa kwenye kikosi cha Hispania katika michezo 20 aliyocheza, amekuwa na uwezo wa juu sana wa kufunga aina mbalimbali ya mabao yakiwemo yale ya adhabu ndogo lakini akitajwa kama mchezaji ambaye anaweza sana kucheza soka la kasi.
Tayari kocha wa timu hiyo ameshapata kiburi kwa kusema kuwa timu hiyo haitakuwa na mshambuliaji wake, Diego Costa, kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kutokana na uwepo wa staa huyu. Kwenye maisha ya soka ya mshambuliaji huyo ambaye alifanikiwa kuitumikia Juventus kwa misimu miwili, amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 271 na kufunga mabao 103 kwenye ngazi ya klabu

Post a Comment