ad

ad

URAIA WA KARIA UMEKUWA SERA TFF

[caption id="attachment_157755" align="aligncenter" width="684"] Makamu wa Rais wa TFF, ambaye sasa anakaimu nafasi ya urais wa shirikisho hilo, Wallace Karia. [/caption]
KWA mwonekano Wallace Karia hana tofauti na raia wengi wa Somalia, ninamaanisha Wasomali. Ninaamini wako viongozi wengi wa soka, serikalini na sehemu mbalimbali wana mwonekano kama raia wengine wa Somalia na suala la kwamba ni raia wa Tanzania, halina shaka hata kidogo.

Anayeweza kufanya kazi ya kukagua fulani ni raia au la, ni Idara ya Uhamiaji na si vinginevyo. Kawaida watu wanaweza kuwa na asili tofauti za nchi mbalimbali na wakawa Watanzania kama ilivyo kwa Karia ambaye ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu.
[caption id="attachment_157756" align="aligncenter" width="640"] ...Akiongea jambo.[/caption]Karia ni mtumishi wa serikali na aliwekewa pingamizi wakati wa usaili wa uchaguzi huo, kwamba si raia. Mwisho aliyeweka pingamizi, alishindwa kuthibitisha alichokipinga na Karia ambaye ni Makamu wa Rais wa TFF, ambaye sasa anakaimu nafasi ya urais wa shirikisho hilo, akapitishwa.

Lakini kwa sasa inaonekana suala lake linataka kugeuka na kuwa mjadala mkuu wa uchaguzi mkuu wa TFF badala ya sera na mambo sahihi ambayo wapenda mpira au wataka maendeleo ya mpira wangependa kuyasikia.

Wanaogombea wakiwemo wanaochuana na Karia, wanaonekana kutaka kuligeuza suala hilo ni silaha na mbaya zaidi hata wale ambao hawakuweka pingamizi wanaling’ang’ania na kutaka liwe mjadala mkuu. Kama kweli kuna mtu ana uhakika Karia si raia, ni vizuri akalifi kisha suala hilo sehemu husika na baada ya hapo aliache walifanyie kazi kwa kuwa wao ndiyo wanataalamu wa uhakika wa kujua fulani ni raia au la tena kwa uhakika badala ya taarifa za mitaani. Karia alisisitiza ni raia wa Tanzania ingawa alikubali ana asili ya Somalia.

Sasa kama kuna anayejua zaidi, vizuri akawasaidia Idara ya Uhamiaji kama raia mwema ili wafanye kazi yao. Lakini suala la uchaguzi, vizuri mkajikita na nini mtafanya na mtaleta maendeleo yapi katika mchezo wa soka. Hakika kikubwa wadau tunaangalia nani ataleta maendeleo na hili ndiyo jambo kubwa zaidi kuliko rangi, kabila au jambo fulani la mtu. Suala la uadilifu linaweza kuwa muhimu pia kwa kuwa tumeona namna viongozi wengi walio kwenye mpira ambavyo wamekuwa wakitafuna fedha za mpira bila ya aibu hata kidogo na wengi wamekuwa wakiona kama ni haki kufanya hivyo na wanapozuiwa au kukosolewa basi wanaona kama wanaonewa au kudhalilishwa.

Tuwe na haya, tuone aibu kwa kuwa viongozi mliopita na wengi mpo mnagombea TFF mmeuumiza sana mpira wetu mkiwa katika klabu au hata shirikisho. Basi safari hii lazima mjue watu wanataka maendeleo, wanataka mabadiliko na hivyo wekeni sera, semeni mtaleta nini kuliko kung’ang’ania hoja ambazo hazihusu mpira na kuzigeuza hoja zinazotemewa au zitakazoujenga mpira wa Tanzania ambao unahitaji msaada na watu sahihi kuliko blabla.
STORI: SALEH ALLY, CHAMPIONI

No comments

Powered by Blogger.