Rammy Aopoa Kifaa Cha Gambia
STAA wa filamu Bongo, Rammy Gallis amenasa kifaa kipya kutoka nchini Gambia ambaye naye ni msanii wa filamu, Princess Shyngle na kusema kuwa mwanadada huyo ndiye anayemkonga nyoyo kwa sasa japo hapendi kumuuzisha sura.
Akipiga stori na Star Mix baada ya meseji za mapenzi akichati na mwanadada huyo kunaswa na paparazi wetu, msanii huyo alifunguka kuwa, yupo kwenye uhusiano na mlimbwende huyo kwa muda sasa na kwamba miongoni mwa vitu vilivyomvutia kwake ni pamoja na figa matata aliyonayo.
“Nilikutana na Princess nilipoenda kufanya filamu Nigeria, kwa kuwa yeye ni Mgambia lakini makazi yake makubwa ni Nigeria, nampenda sana naamini yeye ndiye tulizo la moyo wangu, mapenzi ya Kibongo yanitue kwa sasa,” alisema.
Post a Comment