Jose Mourinho Anamwaga Fedha za kusajili
Mourinho hajawahi kuwa na aibu katika suala la matumizi ya fedha za kusajili, kwake suala la kuwataka mabosi wake kumwaga fedha nyingi kumpata mchezaji anayemtaka siyo kitu kigumu kwa kuwa amekuwa akifanya hivyo kisha mtihani unabaki wake kuhakikisha anatwaa mataji.
Inaelezwa kuwa Matic anaweza kusajiliwa kwa pauni milioni 35, dau ambalo linaonekana ni nono.
Kutokana na hali hiyo, tujikumbushe wachezaji wanaoweza kuunda kikosi kwa kila nafasi waliosajiliwa kwa gharama kubwa na kocha huyo.
Kipa Asmir Begovic, Chelsea Pauni 8m (2015)
Alisajiliwa akitokea Stoke City, bahati nzuri k w a Mourinho katika nafasi hii ni kuwa makipa wengi aliowakuta kwenye timu alizofundisha walikuwa na uwezo mkubwa, h i v y o h a k u t u m i a gharama kubwa kusajili mbadala.
Baadhi ya ‘majembe’ aliyoyakuta ni Petr Cech, Iker Casillas na David De Gea.
Beki wa kulia Paulo Ferreira, Chelsea Pauni 13.2m (2004)
A l i k u w a mmoja wa mabeki hodari wa kocha huyo amb a y e a l i f a n y a kazi nzuri alipokuwa Chelsea. Kwenye nafasi hii pia hajatumia fedha nyingi kwa kuwa huyu alimsajili miaka 13 iliyopita.
Beki wa kati Eric Bailly, Manchester United Pauni 30m (2016)
Aliposajiliwa jina lake halikuwa maarufu sana, lakini kwa sasa watu wote wa soka wa England na Ulaya wanamjua vizuri kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha ndani ya msimu mmoja.
Beki wa kati Victor Lindelof, Manchester United Pauni 31m (2017)
Beki mpya kutoka Benfica ambaye hajagusa hata nyasi za uwanjani akiwa kwenye jezi yake hiyo mpya.
Inaonekana Mourinho anajua anachokihitaji kutoka kwake, wengi hawana ufahamu mkubwa juu yake lakini inavyoonekana anaweza kufiti, japokuwa hilo ni deni kubwa kwake.
Beki wa kushoto Fabio Coentrao, Real Madrid Pauni 26.5m (2011)
Baada ya kuonyesha uwezo mzuri akiwa ndani ya Benfica na katika michuano ya Kombe la Dunia ya 2010, Coentrao alielekea Madrid kujiunga na Mreno mwenzake. Bahati mbaya uwezo wake ukawa wa kawaida na hakupata mafanikio makubwa kama ilivyotegemewa.
Kiungo wa kulia Willian, Chelsea Pauni 30m (2013)
Ni aina ya wachezaji ambao wanaonekana hawana vipaji vikubwa lakini ni wepesi wa kujifunza na kujituma. Alikuwa mtumishi mwenye kuaminiwa kwa kocha huyo ambaye alikuwa akimtumia katika mechi muhimu kwa kumpa majukumu ya kukaba na kushambulia.
Kiungo wa kati Paul Pogba, Manchester United Pauni 89m (2016)
Ukitaja jina la Pogba unataja fedha. Mchezaji ghali zaidi duniani ambaye usajili wake ulizua gumzo kutokana na kuonekana kama thamani yake imekuzwa kupitiliza.
Alirejeshwa klabuni hapo baada ya kuondoka akiwa mdogo, akapewa mzigo mkubwa wa kutakiwa kuishi kwenye thamani ya fedha aliyosajiliwa, amekuwa na msimu mzuri japo kuna wakati alipata wakati mgumu uwanjani.
Kiungo wa kati Luka Modric, Real Madrid Pauni 33m (2012)
Kiungo fundi ambaye usajili wake ulizua gumzo kutokana na Spurs kusita kumuuza, aliposajiliwa alionyesha ufundi kwenye kuuchezea mpira na mpaka sasa bado ni tegemeo kwenye kikosi cha kwanza.
Kiungo wa pembeni Henrikh Mkhitaryan, Man United Pauni 26.3m (2016)
Alianza kwa kuwa na maisha magumu kutokana na kutozoea mazingira, mara kadhaa alilaumiwa na kocha wake lakini baadaye alianza kuzoea mazingira na kucheza soka zuri.
Mshambuliaji Diego Costa, Chelsea Pauni 35m (2014)
Mourinho amekuwa na kawaida ya kuwa na straika mmoja matata ambaye ni tegemeo. Ndiyo ilivyokuwa kwa Costa, alimsajili licha ya kuonekana alikuwa ni mchezaji mkorofi, lakini alipata mafanikio na kuwa staa wa Chelsea.
Mshambuliaji Andriy Shevchenko, Chelsea Pauni 30m (2006)
Alisajiliwa kwa gharama kubwa licha ya kuwa hakuwa chaguo la Mourinho, matokeo yake akawa na maisha magumu na mbinu za kocha huyo hazikumsaidia kuamka na kurejesha enzi zake kama ilivyokuwa.
MANCHESTER, England
Post a Comment