- Alvaro Morata akiwa na bibi harusi wake, Alice Campello, jana jijini Venice.
MCHEZA
soka wa Real Madrid, Alvaro Morata, ambaye anawaniwa vikali na klabu za
Manchester United na AC Milan, jana alimwoa mchumba wake, Alice
Campello, huko Venice, Italia.
- Mora na Alice wakionyesha penzi lao.
Morata
mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na Madrid akitokea Juventus,
anasemekana hana uelewano mzuri na kocha wake, Zinedine Zidane. Hata
hivyo, ndoa yake iliyofanyika katika kanisa la Basilica de Redentore
iliwasahaulisha watu wengi uvumi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa
Hispania kuhusu kuihama klabu yake ya sasa.
Shamrashamra za harusi ya Morata na Alice.
Post a Comment