Kumnunua Ronaldo ni Sh. Trilioni 1.3 Waambiwa Man U, PSG
REAL MADRID imesema inaweza kupokea Paundi milioni 350 ambazo ni sasa na Sh. Trilioni 1.3 ili kumruhusu mchezaji wao Cristiano Ronaldo kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu za Paris Saint-Germain au Manchester United.
Mchezaji mwenye umri wa miaka 32 hana furaha ya kuweko kwake na klabu hiyo ya Bernabeu kutokana na kutoungwa mkono katika mapambano yake na mamlaka za kodi za Hispania, pia kile anachoona kutotendewa haki na vyombo vya habari na kuzomewa kwa mara kwa mara ambako amekuwa akifanyiwa na mashabiki wa Real Madrid.
Dau la kuuzwa kwake limepangwa kuwa ni Pauni 870, kiwango ambacho hakuna klabu yoyote inayoweza kulitoa, zikiwemo za China. Hata hivyo, Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, amesema klabu yake inaweza kuchukua Pauni milioni 350 ili kumuuza Ronaldo.
Post a Comment