MKE MDOGO WA MZEE YUSUF AZIKWA KISUTU NA MAMIA
MAMIA ya waombolezaji leo wamemzika marehemu
Chiku Hamisi aliyekuwa mke wa mwimbaji taarab aliyestaafu na kumrudia Muumba
wake, Ustaadhi Mzee Yusuf. Chiku
aliyezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo mchana, alifariki dunia
katika Hospitali ya Amana jijini Dar Jumamosi jioni ambapo alikwenda kujifungua.
Chiku alipoteza maisha akisaidiwa na wauguzi
kujifungua kwa njia ya upasuaji ambapo
mwanaye aliyekuwa tumboni alifariki pia.
Shughuli za msiba na mazishi zilianzia
nyumbani hapo Kariakoo Mtaa wa Amani na Livingstone ambapo mwili ulitolewa nyumbani hapo na kwenda kuswaliwa
kwenye msikiti wa Manyema.
Baada ya suala mwili ulipelekwa makaburi ya
Kisutu jijini hapa.
Katika mazishi hayo Mzee Yusuf alishindwa
kuzungumza chochote baada ya kuishiwa nguvu ambapo aliondolewa makaburini hapo
kwa msaada wa waombolezaji.
Na
Richard Bukos/GPL
Post a Comment