Mkurugenzi wa Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amtoa Machozi Rais Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli amesema
amepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa benki ya AFDB
Dkt Tonia Kandiero kilichotokea usiku wa jana, na kusema kwamba ni mtu
aliyechangia maendeleo Tanzania.
Rais
Magufuli ametuma salamu hizo za rambirambi kwa Rais wa benki hiyo
Akinwumi Adesina na kusema kuwa Dkt Tonia atamkumbuka kama hodari na
mchapakazi katika kipindi cha uhai wake na kwamba kwa kushirikiana kwao
kulifanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa iliyokuwa chini ya ufadhili
wa AFNB.
Kifo cha Dkt Tonia kimetokea usiku wa jana Juni 28 alipokuwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika kusini.
Post a Comment