Cristiano Ronaldo Apata Watoto Mapacha
Saa
kadhaa baada ya kuiongoza Ureno katika mechi ya nusu fainali ya kombe
la mashirikisho ambapo ilishindwa nchini Urusi, Cristiano Ronaldo
ametangaza kupata pacha.
Siku
nne zilizopita vyombo vya habari nchini Ureno vilitangaza kuwa pacha
wake walizaliwa kutoka kwa mama aliyejitolea kushika mimba kwa niaba ya
mkewe nchini Marekani.Lakini ni baada ya timu yake kuondolewa katika mashindano hayo kwa njia ya penalti na chile ndiposa akathibitisha kuzaliwa kwa pacha hao.
Ronaldo aliandika katika facebook: Nina furaha chungu nzima,hatimaye kuwa na watoto angu kwa mara ya kwanza.tayari ana mwana wa kiume, Cristiano Ronaldo Junior ambaye alizaliwa mnamo mwezi Juni 2010.
Mshambuliaji huyo wa Real madrid alianza ujumbe wake kwa kutangaza kwamba aliichezea timu yake ya taifa kwa moyo wake wote licha ya kushindwa kufanikiwa.
Mechi hiyo ya nusu fainali iliochezwa mjini Kazan iliisha 0-0 huku Chile ikishinda kupitia mikwaju ya penalti ambapo wachezaji watatu wa Ureno walikosa kufunga.
Post a Comment