IKIWA
imepita miezi michache tangu ajiapize kuwa hatakuja kujichora tattoo ya
mwanaume yeyote atakayekuwa naye katika uhusiano, muuza sura kwenye
video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’
ameumbuka baada kunaswa akiwa amejichora jina la mwandani wake, Mourad
Alpha ‘Moj’.
Mourad Alpha ‘Moj’.
Mwanadada
huyo ambaye mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mgogoro na Moj kwa
madai kuwa amekuwa akimpiga bila sababu za msingi hivyo anatumia nguvu
kubwa kuachana naye lakini anashindwa, amejikuta akiumbuka kwa kujichora
tattoo ya jina lake. Alipobanwa baada ya kunaswa na tattoo hizo, Gigy
alisema; “Haa unaniuliza, sijui hata nikujibu nini? Nguvu ya mapenzi
ndiyo imenisababisha kufanya hivi, migogoro ni kawaida katika mapenzi na
kupigwa kila wakati nimeshazoea.
Post a Comment