Emmanuel Okwi Mfano Wa Watu Wenye Vipaji Vya Biashara
Si mwoga na haogopi kuvunja biashara anapoona hakuna biashara. Kwa hapa nyumbani, wafanyabiashara wanaojulikana kwa kujitolea na kutaka kufanikisha wanachotaka ni ndugu zetu wa Kabila la Wachaga. Hawa huanza na duka dogo hadi linakua na baadaye wakawa matajiri ya tatu tokea alipojiunga nayo mwaka 2009 kwa mara kwanza akitokea SC Club Villa ya Uganda akiwa kinda mwenye miaka 17 tu.
Simba ilimnunua kwa dola 20,000 (zaidi ya Sh milioni 40) akitokea SC Villa, nayo i k a m u u z a Etoile du Sahel ya Tunisia kwa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 660). Tunisia Okwi hakudumu, akavunja mkataba na kurejea SC Villa ambako aliweza kuweka kituo hadi aliponunuliwa na Yanga kwa dola 35,000 (zaidi ya Sh milioni 77) ambako hakudumu pia hadi alipoamua kurejea Simba akiwa huru na kusajiliwa kwa dola 20,000 tena. Simba ilikaa naye na ndani ya msimu ilishapata biashara na kumuuza Sonderjysker ya Denmark kwa kitita cha dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 221).
Sasa ametua Simba na kuchota kitita hicho cha dola 50,000 akiwa anakamilisha kuhama mara nane tokea 2009. Kila uhamisho akiwa ameingiza fedha na pia kaiingizia Simba dola 400,000 (zaidi Sh milioni 884). Simba imegharimika dola takribani 100,000 kumnasa mara zote tatu alizojiunga nayo. Mara moja 20,000 halafu 20,000 tena na 50,000 lakini kuna fedha amba
zo hutoka katika ukamilishaji wa mikataba.
Hivyo, Simba ndiyo imepata faida zaidi kwa kuwa inaonekan a faida yake kwa Okwi ni dola 300,000. Utaona namna Okwi anavyoweza kucheza na “mapengo” ya kutengeneza biashara wakati anatoka timu moja kwenda nyingine.
Lakini angalia alivyo mjanja pale anapovunja mkataba na timu moja, haraka anakuwa huru na anaporejea Villa anapiga soka kweli na kutengeneza kiwango. Anapopata timu, basi anakuwa na nafasi ya kuchota dau kubwa.
Anawagawia Villa kidogo anakwenda kupiga kazi. Baada ya msimu mmoja, mwisho miwili lazima atapata soko na ikishindikana anavunja mkataba.
Hata hivyo inaonekana hivi, amevunja mkataba kutoka timu zenye fedha nyingi kama zile za Ulaya na Amerika Kusini. Na kutoka katika timu amb a z o hazina u w e z o mkubwa sana, huko anajituma na kupata soko la kuuzwa. Okwi anakuwa uwanjani lakini anajua anachokifanya kwa ajili ya ‘ku-market’ au unaweza kusema hivi; '’Okwi ni Ofi sa Masoko wa Okwi”.
Post a Comment