ad

ad

SPORTPESA YAIBUKA NA MICHUANO YAKE, SIMBA, YANGA NDANI

Katika kile ambacho kinaonekana kufanya mapinduzi ya soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla, Kampuni ya SportPesa, leo Jumatano imezindua ligi itakayojulikana kama SportPesa Super Cup.
Ligi hiyo itashirikisha timu nne za Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa.
Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza  Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11.
“Utakuwa ni ushindani wa timu nne, kutoka Tanzania na Kenya. Hawa ni majirani na siku zote ni wapinzani wakubwa,” alisema.

Bingwa wa SportPesa Super Cup atabeba 30,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 66 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000 zaidi ya shilingi milioni 22.

Ikumbukwe kuwa kampuni hiyo imeshatangaza kuzidhamini Simba, Yanga na Singida United zote za Ligi Kuu Bara msimu huu.

RATIBA KAMILI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017
Timu za Tanzania.
1. Simba.
2. Yanga
3. Singida United Fc
5. Jang'ombe Boys (Zanzibar).

Timu za Kenya
1. Golmahia
2. Tusker Fc
3. FC Leopard
4. Nakulu

Juni 5, 2017
AFC Leopards Vs Singida United
Saa 8:00 Mchana.

Yanga Vs Tusker
Saa 10:00 Jioni

Juni 6, 2017
Simba Vs Nakulu
Saa 8:00 Mchana

Gol Mahia Vs Jang'ombe
Saa 10:00 Jioni

UWANJA WA UHURU, DAR ES SALAAM

Nusu fainali
Juni 8, 2017
Mshindi wa Singida United vs AFC Leopards atacheza na mshindi wa Yanga Vs Tusker.

Nusu fainali ya pili mshindi wa mechi Simba VS Nakuru All Stars atacheza na Jangombe Boys Vs Gor Mahia.

Fainali
Juni 11, 2017

No comments

Powered by Blogger.