Breaking News: FIFA Yaipongeza Yanga Kwa Ubingwa Ligi Kuu Bara
RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino,
ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Yanga baada ya kuwa mabingwa Ligi
Kuu Bara msimu wa 2016/17.
Fifa imeipongeza Yanga baada ya kumaliza msimu ikiwa kileleni na pointi 68 ambazo ni sawa na za Simba, lakini Yanga imeweza kuwa bingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambayo ni kumi.
Salamu za Fifa kwa Yanga zimewasilishwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi baada ya leo kuandika kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter.
Wakati Fifa inaipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa huo, watani zao wa jadi, Simba bado wanadai kupewa pointi zao tatu ambazo awali walipewa na Kamati ya Saa 72 kutokana na kumkatia rufaa beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi ambaye anadaiwa kucheza dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1.
Baada
ya Simba kupokwa pointi hizo na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji, viongozi wa klabu hiyo wakaenda kukata rufaa Fifa ambapo
mpaka shirikisho hilo linatuma pongezi zake kwa Yanga kuwa bingwa, bado
Simba haikuwa imepewa majibu ya rufaa yao kama imeshinda au la.

Post a Comment