POGBA AANZA MFUNGO WA RAMADHANI AKIWA SAUDI ARABIA, AKITAJA KILICHOMPELEKA
Staa wa Manchester United, Paul Pogba amesafiri hadi nchini Saudi Arabia ikiwa ni muda mfupi baada ya kuiwezesha timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa Europa League.
Pogba amesafiri hadi nchini humo ikiwa ni mwanzo wa mfungo wa Ramadhani kwa waumini wa dini ya Kiislam.
Jumatano iliyopita, Pogba alifunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ajax katika fainali hiyo jijini Stockholm nchini Sweden.
Picha zimemuonyesha Pogba akiwa katika mavazi meupe sawa na waumini wengine.
Bado haijajulikana mchezaji huyo atautumia muda wake wote wa mapumziko nchini humo au la.
Kabla ya kuondoka Manchester, aliweka video fupi akiwa na begi mtandaoni na kuandika: “Najiandaa kwenda kusema asante kwa kilichotokea msimu huu, tutaonana baadaye watu wa Manchester!”
Post a Comment