Nape Nnauye Amvaa Tena Mkuu wa Mkoa Sakata la Kuvamia Clouds Media
IKIWA
ni miezi miwili imepita tangu kutokea tukio la uvamizi wa kituo cha
Clouds Media Group na kuundwa kwa kamati ya kuchunguza tukio hilo,
hatimaye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye amemvaa tena Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba
hakuunda kamati ya kumchunguza yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza
tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji cha Clouds Media Group.
“Niliunda
kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio
kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya
sheria,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Alipoulizwa
kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi
badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Nape
alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Majibu
haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni yapi
maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka yake
ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.
Kauli
ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24 tangu
Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.
Makonda
alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na Waziri
isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na wajumbe
wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya uvamizi.
Post a Comment