Mawaziri na Manaibu Walioteuliwa Juzi Kuapishwa Jumatatu
Tarehe 23 Desemba, 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli aliwateua Mawaziri wanne, Naibu Waziri mmoja na
kumhamisha Wizara Waziri mmoja.
Walioteuliwa ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.
Rais Magufuli pia
alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.
Kufuatia uteuzi huu, Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anawaarifu Mawaziri wote na Naibu Waziri
walioteuliwa kuwa wataapishwa Jumatatu tarehe 28 Desemba, 2015 Saa
tatu asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
24 Desemba, 2015
Post a Comment