JAMANI DADA MARTHA LOOO!-16

“Martha acha mambo ya utani bwana.”
“Sina utani, anaishi na mimi pale.”
“Mh! Kumbe una mume Martha?”
“Ndiyo Roi. Ndiyo maana uliponiuliza nina mchumba nikakwambia sina kwa sababu nina mume. Sikutaka kukwambia siku za kwanza kwa sababu zangu binafsi.”
SHUKA NAYO MWENYEWE…
“Sababu kama zipi?”
“Nazijua mwenyewe, iko siku nitakwambia.”
“Kama ni hivyo Martha please tuendelee kuwa kaka na dada kuanzia sasa hivi tunavyoongea, mimi si mpenzi wako tena na wala wewe si mpenzi wangu tena.”
“Noo! Roi noo! Mimi bado nakuhitaji wewe kama mpenzi wangu. Ukaka na udada ulishakufa, we unajua.”
“Martha…” aliita Roi.
“Abee…”
“Katika vitu sivitaki katika maisha yangu ni kutembea na mke wa mtu. Sitaki wala sipendi na sitamani. Kwangu mke wa mtu ni sumu kama sumu nyinginezo. Yaani wewe saa hizi ninapokuangalia nakuona kama ile sumu ya kuulia panya,” alisema Roi akiwa amekunja sura.
“He! Hayo yote yanatokana na nini mpenzi wangu jamani?”
“We unajua. Kumbe una mume wako halafu unatembea na mimi! We ni msaliti.”
Martha alimlalia mapajani Roi na kuanza kulia tena kile kilio cha kwikwi.
“Unalia nini sasa?” aliuliza Roi mikono ikiwa juu kwa maana kwamba hakuwa anataka kumshika Martha.
“Baby,” aliita Martha kwa sauti tamu sana…
“Nini?”
“Kuna kitu nilitaka kujifunza kwako.”
“Kipi?”
“Niliamua kukudanganya ili nione kama utakubali kuendelea kuwa na mimi au la! Inaonekana wewe ni mwanaume mwaminifu, usiyetaka kuchanganya. Nimefurahi sana,” alisema Martha…
“Martha we mwongo. Unajifanya ulikuwa unanidanganya kwa vile nimekuonesha msimamo wangu siyo? We si mkweli.”
“Baby, unataka nifanyeje ili uamini?”
“Mimi sijui ufanyeje! Wewe ndiyo unajua ufanyeje!”
“Twende ukalale kwangu leo,” alisema Martha huku akimwangalia Roi kwa kutokea chini.
Sasa Roi alishalegeza masharti. Alimshika mwilini Martha huku akimpapasapapasa sehemu mbalimbali. Mara kifuani, mara tumboni, mara kwenye nido.
“Pengine mumeo kasafiri.”
“Utawauliza wale wanawake.”
“Ah! Si utawaambia hata kwa simu kwamba nikiwauliza wajibu nini!”
“Basi twende kwako nikalale huko.”
“Sitaki. Si utamdanganya mumeo kwamba umekwenda kumsalimia shangazi yako.”
“Jamani baby! Sasa nifanyeje ili uamini nilikuwa nakudanganya?”
“Mimi sijui Martha.”
“Haya! Sikia, basi twende kwako, chukua nguo, twende kwangu. Ukae pale hata kwa siku kadhaa hivi.”
“Sawa. Twende.”
Roi na Martha waliondoka mpaka nyumbani kwa Roi. Ilikuwa mara ya kwanza, Martha kuingia kwenye nyumba hiyo, akapongeza kwa jinsi ilivyo.
Roi alibeba nguo za kubadili kwa siku tano, aliamini ndani ya siku hizo. Atajua ukweli kwa kuchunguza mambo kadhaa.
Walianza safari hadi nyumbani kwa Martha…
“Hilo duka lina mlinzi baby, kwa hiyo gari laza hapahapa nje,” alisema Martha. Mbele ya nyumba anayoishi kuna barabara, ng’ambo yake kuna duka.
Ilikuwa ni dalili ya kwanza kwa Roi kuthibitisha kwamba, kweli Martha hana mume…
“Angekuwa ana mume, asingetaka gari lilale jirani hivi,” alisema moyoni huku akifunga milango.
Nje ya nyumba, walikaa wale wapangaji wenzake, Martha. Walipomwona Roi walimchangamkia sana…
“Karibu kaka…mzima wewe? Za siku jamani?”
“Njema…njema…njema sana,” Roi aliwaitikia wote kwa kuunganisha maneno.
Walipoingia ndani, nyuma maneno yakaanza…
“Jamani, mbona kaja na begi? Ndiyo kahamia nini?”
“Inawezekana. Lakini jamani twende mbele na kurudi nyuma, Martha si mwanamke machepele,” alisema mmoja wa wapangaji hao.
“Ni kweli. Ila aliwahi kuwa na kizee kimoja hivi, sijakiona muda, nadhani walizinguana,” alisema mwingine.
Wapangaji hao walimchambua Martha mpaka wakafika kwa Roi, kwamba kwa nini anamtambulisha kama kaka yake wakati ni mpenzi wake?
“Kile kizee alikitambulisha kuwa ni mpenzi wake, sasa huyu kijana mwenzake kwa nini anasema ni kaka yake?” aliuliza mpangaji mmoja.
“Ukiona hivyo ujue ni mume wa mtu. Kile kizee si kilifiwaga na mke, ndiyo maana alikiweka wazi,” alisema mpangaji mwingine. Mpangaji wa tatu akatahadharisha kuwa, Martha anatoka baada ya kusikia kutembea kwake…
“Anakuja jamani… anakuja! Nyamazeni.”
Martha alitoka na Roi, wakasimama…
“Jamani! Huyu bro wangu atakuwa hapa kwangu kwa siku kadhaa. Kwa hiyo msishangae mkimwona anaingia na kutoka,” alisema Martha kwa sauti ya kujiamini sana kisha akamshika mkono Roi na kurudi naye ndani huku wale wapangaji wakisema…
“Sawa, karibu bro. Hakuna shida.”
Nyuma, walianza tena wale wapangaji…
“Jamani…Martha si ana chumba kimoja tu?”
“Ndiyo.”
“Sasa kaka yake atamlaza wapi?”
“Si anatuvunga tu.”
“Sasa mimi nitamkomesha,” alisema mpangaji mmoja.
“Utamkomeshaje?”
“Nitachukua namba yake ya simu halafu nitaanza kujigonga kwake.”
***
Ulikuwa ni usiku wa kwanza kwa Martha na Roi kulala pamoja wakiwa wamefuta ukaka na udada wao.
Martha ndiye aliyekuwa mchokozi pale kitandani. Alimshikashika Roi kwa kuanzia kichwani, akaja kifuani, akampa kidole chake kwenye kinywa, Roi akakipokea, akamlalia kifuani huku akianza kuhema kwa staili ya mahaba.
Mara, mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni uligongwa…
“Mh! Martha! Si jamaa yako huyo kweli?”
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma chombezo hili tamu sana...
Baada ya kusoma simulizi hii akikisha unashare kuwawezesha marafiki zako kwenda na sisi katika simulizi hii hapa. Share tukutumie sehemu inayofuata mbele.
Post a Comment