Mapenzi Yanawazidi Nguvu Izzo Buzness na Abela Music
- Wanamuziki wawili Emmanuel Simwenga ‘Izzo Buzness’ na mwanadada anayefahamika zaidi kwa jina la Abela Music.
YAWEZEKANA
kukawepo maneno mengi ya kuzungumza juu ya ukaribu wa wanamuziki wawili
Emmanuel Simwenga ‘Izzo Buzness’ na mwanadada anayefahamika zaidi kwa
jina la Abela Music, lakini kubwa ni juu ya kuhusishwa kwa wawili hawa
kuzama kwenye dimbwi la mahaba. Tetesi juu ya mkali huyu wa michano
Bongo kutoka na Abela zilianza kusambaa muda mfupi tu baada ya yeye
kumdaka mwanadada huyo kutoka Ughaibuni alikokuwa anaishi kwa ajili ya
masomo na kuunda kundi wakijiita The Amaizing.
BUZNESS AKANA UHUSIANO
Hata
hivyo tetesi hizo za kutoka na Abela, ‘mzee baba’ Buzness amezikanusha
mara kadhaa. Muda mwingine amekuwa mkali na kudai watu wanashadadia kitu
ambacho si kweli. Kwamba yeye na Abela wapo kwa ajili ya kazi tu na
baada ya hapo kila mmoja wao ana maisha yake mengine, jambo ambalo
linapingana na vitendo pamoja na mienendo yao.

VITENDO VYAWAUMBUA
Mbali
na Buzness kukanusha kutoka na Abela vitendo vinawaumbua. Ukweli ni
kwamba wawili hawa ni kama kumbikumbi. Muda mwingi wanakuwa pamoja.
Katika
kazi na sehemu tofautitofauti wakila bata na wanaowafahamu zaidi
wanasema hata anapoishi Buzness mitaa ya Sinza B, mwanadada huyo
anaonekana mara kwa mara jambo ambalo linazidi kuzua maswali zaidi. Acha
na hayo, hivi karibuni Buzness na mwanadada huyo walikuwa kwenye shoo
ya mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Fid Q pale kwenye Ukumbi wa Next Door,
Masaki Dar. Wakiwa pale walionekana kuwa karibu mno.

Lakini
kilichowafanya watu wapigie mstari tetesi juu ya wawili hao ni namna
Izzo alivyokuwa anamkumbatia na hata alivyopanda jukwaani
alipokaribishwa kuwasalimia mashabiki. Buzness alimpandishi mwanadada
huyo pia jukwaani na kumtambulisha kuonyesha mahaba ‘live’ akimkumbatia
na kuwauliza mashabiki walikuwa wanawaonaje.

MAPENZI YAWAZIDI NGUVU
Kutokana
na hali halisi hivi ndivyo unaweza kusema. Inawezekana kabisa Buzness
anajaribu kuficha juu ya uhusiano wake na Abela kwa masilahi fulani.
Lakini
ukweli ni kwamba mapenzi yamewazidi nguvu na kama walivyosema Waswahili
mapenzi ni kama kikohozi huwezi kuficha, limekuwa ni suala gumu kwa
mkali huyo kuendelea kuwapiga kamba watu kuwa habanjuki kimalavidavi na
Abela.
Post a Comment