ad

ad

WAMEBANA WAMEACHIA YANGA BINGWA, HAWA NDIYO YANGA IMESHINDA MECHI NYINGI VPL

 

HEBU piga picha, pale unapofikiri umening’inia kwenye mti na kuepuka shimo halafu ghafla mti unakatika na unatumbukia shimoni! Hivyo ndivyo alivyofanya straika Mrundi, Amissi Tambwe mbele ya mamia ya mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Ilikuwa ni wakati Toto Africans wakiamini wamepata pointi moja muhimu mbele ya Yanga
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kubana weeee, lakini ghafla dakika za mwisho Tambwe akawararua na kupoteza matumaini yao ya kusalia kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kichapo hicho cha bao 1-0.


Bao hilo la Tambwe lililiza watu wenye rangi mbili. Kwanza, ni wale wenye rangi nyekundu na pili, ni wale wenye rangi za njano za Kimwanzamwanza, kwani matokeo hayo yanamaanisha kuwa ubingwa kwa Simba sasa ni ‘byebye’. Hakuna tena nafasi kwa Simba kutwaa ubingwa msimu huu. Yanga wamefikisha pointi 68, wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku kila timu ikiwa imebakiza mechi moja ligi iishe. Simba wana pointi 65 na sasa watalazimika kushinda zaidi ya mabao  12-0 katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mwadui, ikimaanisha kwamba hakuna tena ubingwa msimu huu walioukosa tangu mwaka 2012. 


Bingwa ni Yanga. Matumaini pekee ya Simba ni pointi tatu za mezani watakazozifuatilia Fifa lakini kama Yanga asiposhinda mechi ya mwisho dhidi ya Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kama Yanga akishinda, pointi hizo zinakuwa hazina maana tena. Kwa upande wa Toto, ili kusalia ligi kuu, watalazimika kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro huku wakiombea wapinzani wao wote katika vita ya kuporomoka daraja, wasipate matokeo mazuri, vinginevyo ni kilio kwa Wanamwanza. Timu hiyo inabaki katika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 30. Bao la Tambwe alilifunga dakika ya 79 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Juma Abdul. 

Bao hilo lilipatikana baada ya Yanga kulisakama lango la Toto kwa muda mrefu bila mafanikio. Tambwe sasa anafikisha mabao 11 kwenye chati ya wafungaji na amebakiza mabao manne amfikie Yanga mwenzake, Simon Msuva ambaye hakucheza jana kutokana na majeraha na kuna hatihati ya kucheza tena msimu huu. Baada ya mchezo huo, wachezaji wa Yanga walizunguka uwanja mzima wakishangilia ubingwa ambao dhahiri kabisa sasa ni wao

No comments

Powered by Blogger.