ad

ad

FT: YANGA 1-0 TOTO AFRICANS, UWANJA WA TAIFA, YANGA MABINGWA


FULL TIME
Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inaibuka na ushindi wa bao 1-0.
Dakika ya 94: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Haruna Ninyonzima, anaingia Justine Zullu.
Dakika ya 92: Kasi ya mchezo imepungua, wachezaji wa Toto wanaonekana wakilaumiana wao kwa wao mara kadhaa.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.
Dakika ya 88: Beki wa Yanga, Juma Abdul yupo chini na mchezo umesimama kwa muda.
Dakika ya 87: Yanga wanafanya shambulizi lingine kali, Chirwa anapata nafasi ya kufunga lakini anashindwa kutumia vizuri.
 
Dakika ya 70: Yanga wanamtoa Mwashiuya, anaingia Emmanuel Martine.
Dakika ya 65: Timu zote zinaendelea kushambuliana kwa zamu. Bossou anapanda mbele kusaidia mashambilizi, Yanga wanapiga pasi ndefu.
Dakika ya 62: Waziri Jr anawatoka wachezaji wawili wa Yanga, Kaseke na Juma Abdul lakini Bossou anaingia kati na kuokoa.
Dakika ya 60: Yanga wanapata kona kutokana na Haruna Niyonzima kufanya kazi nzuri, inapigwa kona lakini walinzi wa Toto wanaokoa.
MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, timu zote zinaenda kupumzika vyumbani.
Dakika ya 48: Yanga wanafanya shambulizi, kipa wa Toto anafanya makosa lakini mpira unatoka inakuwa kona, inapigwa mabeki wanaokoa.
Dakika ya 47: Washambuliaji wa Yanga, Chirwa na Tambwe wanakosa maelewano mazuri baada ya kusogea na mpira hadi karibu na lango la Toto.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akipa anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 43: Yanga wanaendelea kucheza soka la kuelewana, wnaapiga pasi nyingi.
Dakika ya 40: Yanga wanapata kona kutokana na Chirwa kutumia nguvu kubwa wakati akishambulia.
Dakika ya 40: Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, anapiga shutikali, kipa anapangua inakuwa kona.
Dakika ya 37: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 32: Yanga nao wanajibu mapigo wanatengeneza mashambulizi, Tambwe anaonekana kuana kupambana, Yanga wanamiliki mpira hasa sehemu ya katikati.
Dakika ya 30: Toto wanaonekana kuanza kuelewana na kujipanga kufanya mashambulizi kwa Yanga, wanapata kona.
Dakika ya 26: Toto wanapata kona, wanapiga mpira lakini kipa wa Yanga, Beno anaudaka mpira na kumrushia Chirwa ambaye anaingia nao kwa kasi lakini walinzi wa Toto wanamuwahi.
Dakika ya 25: Lusajo Lerient anapata nafasi nzuri ya kufunga lakini anashindwa kuitumia.
Dakika ya 22: Juma Abdul anafanya kazi nzuri anapanda kushambulia lakini mpira unawahiwa na mabeki wa Toto wanautoa.
Dakika ya 20: Yanga wanamfanya kipa wa Toto, David Kissu kuwa bize kutokana na kufika langoni kwake mara kwa mara.
Dakika ya 15: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini kipa wa Toto anafanya kazi nzuri, anapiga mpira mrefu kuelekea kwa mchezaji wake Wazir Jr.
Dakika ya 10: Chirwa anachezewa faulo.

Dakika ya 5: Toto wanarudi nyuma wachezaji wao kuanza kuzuia.

Dakika ya 2: Yanga wanaendeleza kasi kama kawaida, inavyoonekana wanatafuta bao la mapema.
Dakika ya 1: Yanga waanza kwa kasi
Mwamuzi anaanzisha mchezo
Kabla ya mchezo kuanza, mwamuzi alipuliza filimbi na upande wa timu zote, wakasimama kutoa heshima.
Kikosi cha Yanga ambacho kitashuka uwanjani leo kukipiga dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom tayari kimeshatoka, wachezaji 11 watakaoanza hawa hapa:
1. Beno Kakolanya
2. Juma Abdul,
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamusoko
7. Juma Mahadhi.
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya
Akiba
Deogratius Munishi, Hassan Kessy Nadir Haroub, Matheo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin na Justine Zulu.

No comments

Powered by Blogger.