Hii hapa First Eleven Ya Wachezaji wa Kigeni Ligi Kuu Bara 2016/17
MSIMU wa Ligi Kuu Bara 2016/17 umemalizika wikiendi iliyopita kwa Yanga kufanikiwa kulitetea taji lao walilolichukua kwa mara ya tatu mfululuzo.
Yanga ambayo msimu huu ilikuwa chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina aliyechukua mikoba mzunguko wa pili kutoka kwa Hans van Der Pluijm, wamechukua ubingwa huo wakiwa na pointi 68 sawa na Simba waliokuwa wanaliwania taji hilo ambalo wamelikosa kutokana na kuzidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wakati Yanga wakiuchukua ubingwa huo, jumla ya timu tatu zimeshuka daraja katika msimu huu wa ligi ambazo ni JKT Ruvu, African Lyon na Toto Africans na kuzikaribisha Njombe Mji ya mkoani Njombe, Singida United ya Singida na Lipuli FC ya Iringa katika nafasi zao.
Championi Jumatano, linakuletea First Eleven ya wachezaji wa kigeni wa timu 16 zilizokuwa zinachuana kwenye msimu huu wa ligi kuu.
Ni kipa raia wa Ghana aliyetua kuichezea Simba kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu na kuonyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia klabu yake hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili lakini pia akiipeleka kwenye fainali ya Kombe la FA, Agyei alifanikiwa kuiongoza timu yake kufungwa mabao 17 tu msimu huu.
2.BesAla Bokungu (Simba)
Mchezaji kiraka raia wa DR Congo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za beki kwa kuanzia namba 2, 3, 4 na 5 ambazo akiwa na Simba amezicheza nafasi hizo pale inapotokea mchezaji kapata adhabu ya kadi au majeraha, hana kasi kubwa lakini uzoefu unambeba kwani amewahai kucheza klabu kubwa kama TP Mazembe.
Ni raia wa Zimbabwe aliyejiunga na Azam FC kwenye msimu huu wa ligi kuu, yeye ana uwezo mkubwa wa kupeleka mashambulizi kwenye goli la wapinzani na ndani ya wakati mmoja anazuia hatari golini kwake, hizo ndiyo sifa zilizomuingiza kwenye kikosi hiki.
4.Yakub Mohammed (Azam FC)
Ni beki wa kati tegemeo wa Azam ambaye ni raia wa Ghana, sifa yake kubwa ni fiziki aliyonayo na maamuzi ya haraka katika sehemu sahihi katika kuokoa na kupunguza hatari golini kwake akicheza sambamba na Aggrey Morris. Sifa yake nyingine ni kuwa na kontroo nzuri awapo uwanjani.
Wakati anajiunga na timu hiyo ikiwa inafundishwa na Mholanzi, Hans Pluijm beki huyo raia wa Togo, wengi walimdharau na kutomuamini kutokana na kasi yake ndogo aliyonayo, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda akaaminika na kuwa tegemeo, ni nahodha msaidizi wa tatu badala ya Haruna Niyonzima.
6.James Kotei (Simba)
Ukiwataja viraka bora waliocheza kwa kuzipambania timu zao, kamwe hautasita kumtaja Kotei raia wa Ghana kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye timu yake, kiungo huyo anayemudu kucheza nafasi zote za viungo na beki wa kati alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.
Ni kiungo mchezeshaji raia wa Rwanda anayemudu kucheza namba 7, 8, 10 na 11 akiwa na timu hiyo amezicheza nafasi zote katika mechi tofauti za ligi kuu, ni kiungo hatari mwenye uwezo wa kuuchezea mpira anavyotaka huku akiwa na sifa nzuri ya kukokota mpira, kupiga chenga za maudhi na kupiga pasi za mwisho ‘asisti’.
8.Thabani Kamusoko (Zimbabwe)
Ni kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kuchezesha timu na kupunguza presha ndani ya uwanja wakati ikiwa inashambulia kwa kukaa na mpira, pia umakini wake wa kupiga pasi zenye macho kwa wachezaji wenzake. Ameisadia timu hiyo kutwaa taji la ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo huku yeye akibeba mbili.
9.Obrey Chirwa (Yanga)
Unaweza kusema huyu ndiye shujaa wa Yanga aliyefanikisha ubingwa wa tatu mfululizo kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye timu yake katika mechi hizi za mwisho za ligi kuu, Chirwa raia wa Zambia, alianza kutumika kwenye mechi mfululizo baada ya Mzimbabwe, Donald Ngoma kupata majeraha ya goti ndiyo yeye akapewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza na kumaliza ligi akiwa amefunga mabao 12.
10.Amissi Tambwe (Yanga)
Ni Mrundi aliyewahi kuchukua ufungaji bora mara mbili akiwa na Simba na Yanga na kwenye msimu huu amekuwa wa tatu akilingana na nyota wengine watatu wenye mabao 12 katika orodha hiyo ya ufungaji bora, akiwa uwanjani yeye siyo muongeaji na kikubwa anafanya kazi yake ya kufunga mabao pekee na hatari kwa mipira ya vichwa anapokuwa ndani au nje ya 18 na hiyo ndiyo sababu iliyomuingiza katika kikosi hiki.
Laudit Mavugo (Simba)
Ni mchezaji hatari anapokuwa na mpira kutokana na uwezo wake kukokota mpira huku akiwatoka mabeki wa timu pinzani akitokea pembeni, licha ya kuwa na uwezo wa kucheza namba 9 na 10 katika kikosi cha Mcameroon, Joseph Omog, yeye amefunga mabao saba pekee katika msimu huu wa ligi kuu huku akitengeneza nafasi za kufunga.
Post a Comment