YANGA YAPEWA ONYO KALI, KISA NI MAKOMANDOO WAKE KUVURUGA MAMBO UWANJANI
Mechi namba 195 (Yanga 1 vs Azam 0). Yanga haikuingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo, kutokana na kuwa na maji yaliyomwagwa na wanachama wa klabu hiyo (makomandoo) muda mfupi kabla ya timu hiyo kuwasili uwanjani.
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), ilifanya kikao chake Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao kuhusu tukio hilo.
Kamati imeelekeza Klabu ya Yanga iandikiwe barua ya onyo, na kuitaka kuhakikisha wanachama wake wanaacha mara moja mtindo wa kumwaga maji vyumbani baada ya kuwa vimeshafanyiwa usafi na wafanyakazi wa uwanja tayari kwa ajili ya matumizi ya timu yao.

Post a Comment